Na Mwandishi wetu...
Ofisi ya Hakimiliki Tanzania COSOTA yasaini Makubaliano ya pamoja na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa ajili ya kulipia Leseni za matumizi ya kazi za Muziki katika Viwanja vyote vya Ndege nchini.
Hafla hiyo ya kusaini makubaliano hayo imeshuhudiwa na Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Hamis Mwinjuma na Naibu Waziri Wizara ya Uchukuzi Mhe. David Kihenzile leo Januari 13, 2025 Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma alisema kusainiwa kwa makubaliano hayo ni sehemu ya utekelezaji wa
ahadi ya serikali ya Awamu ya Sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Wasanii wananufaika na matumizi ya kazi zao.
Naye Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. David Kihenzile alieleza kuwa Mamlaka inatambua umuhim wa kulipa gharama hizo na ipo tayari kunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassankatika kusimamia Hakimiliki za Wasanii.
Pamoja na hayo naye Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa hakimiliki Bi.Doreen Anthony Sinare alimshukuru Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bw. Abdul Mombokaleo kwa ushirikano na kuharakisha makubaliano hayo ambayo yatasaidia kuimarisha simamizi wa hakimiliki kwa kazi za Muziki na kuongeza chachu ya ongezeko la makusanyo ya Mirabaha.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bw. Abdul Mombokaleo alipongeza COSOTA kwa kazi kubwa inayofanya ya kusimamia hakimiliki za Wasanii katika kazi zao na Mamlaka itahakikisha 80% ya nyimbo zitakazopigwa ni za Wasanii wa Tanzania na 20% zitakuwa za nje.