Kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA Yusuph Mwenda amesema serikali imejidhatiti kuboresha huduma za forodha katika bandari ya Zanzibar ikiwa ni pamoja na kutumia mifumo ya kisasa katika kukagua na kukusanya kodi na hivyo kuongeza kasi ya ufanyaji wa biashara
Ameyasema hayo jana Wakati wa hafla ya utiaji saini wa hati ya makubaliano baina ya Shirika la viwango Zanzibar (ZBS) pamoja na mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kwa lengo la kubadilishana taarifa baina ya taasisi hizo ili kusaidia katika kurahisisha ufanyaji wa biashara zinaotumia forodha visiwani zanzibar
“Kabla ya makubaliano haya ya kubadilishana taarifa kwenye mifumo, utoaji wa mizigo ulkuwa unachukua muda mrefu hivyo kwa hichi tunachokifanya tunakwenda kupunguza muda wa kutoa mizigo inayopitia bandari ya Zanzibar na ni hatua kubwa ya kurahisisha biashara Zanzbar ambayo inakwenda kupunguza vikwazo na urasimu uliokuwepo” Alisema Mwenda
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi mkuu wa ZBS Yusuph Majid Nassor alisema ZBS imeendelea kushirikiana na TRA hivyo makubaliano hayo yatawezesha kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa kodi za serikali kwa kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wote wanaopitisha mizigo yao katika bandari za Zanzibar wamesajiliwa katika mfumo wa ulipaji kodi
“Kikubwa sisi kwa upande wa Zanzibar tunataka tusimuhudumie mtu yoyote ambaye hana Tin Namba hivyo mkataba huu utahakikisha kuwa wale wote wanaoingiza mizigo kwa upande wa zanzibar amesajiliwa na mamlaka ya mapato na hii maana yake titahakikisha kuwa huyu mtu anakwenda kulipa kodi za serikali kwa usahihi” Alibainisha Yusuph
Naye Naibu Kamishna wa mamlaka ya Mapato Zanzibar Juma Bakari alisisitiza kuwa kusainiwa kwa makubaliano hayo kutawezesha kulinda ubora wa bidhaa zinazoingia nchini na hivyo kulinda afya za wananchi lakini vilevile zinalipiwa kodi stahiki.
“Kimsingi ni makubaliano ambayo yataweza kutubana katika ubadilishanaji wa taarifa ambazo zitawezesha pande zote mbili kunufaika kwa maana ya ukusanyaji wa mapato na upande wa kuhakikisha kwamba bidhaa zinazoingia nchini zinakidhi viwango ili wananchi wasipate madhara yatokanayo na bidhaa hizo” Juma alisisitiza