Waziri wa Nchi Mchengerwa, Ofisini ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) MOHAMMED MCHENGERWA amesema Watu Milioni 31 sawa na asilimia 91 wamejiandikisha katika Daftari ya orodha ya wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27 mwaka huu.
Amesema hayo Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya zoezi la uandikishaji lililoanza rasmi Oktoba 11 hadi Oktoba 20 mwaka huu ambapo amesema kati ya idadi hiyo Wanawake ni zaidi ya Milioni 16 na Wanaume ni zaidi ya Milioni 15 na kwamba Mkoa unaongoza kwa kuandikisha watu wengi ni Mkoa wa Pwani.
Kuhusu maeneo ambayo yalikuwbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo Ofisini zilizokuwa na Madaftari ya orodha ya Wananchi kuchomwa ama kuibiwa amesema tayari Wadau wauchaguzi vikiwemo Vyama vya Siasa vimekaa nakukubaliana kuongeza siku za kujiandikisha ili kila kitu kiweze kwenda vizuri.
Aidha Waziri MCHENGERWA amewasihi Wananchi kuanzia leo kwenda kuhakiki majina ya watu waliojiandikisha na endapo watabaini kuwa wapo ambao hawakustahili hatua zichukuliwe huku akisisitiza Viongozi wa Vyama vya siasa na Wadau wengi kuhamasisha watu kuchukua fumu za kugombea na kwenda kupiga kura pamoja na wasimamizi kuhakikisha wanatoa maelekezo sahihi kwa vyama vyote ili kushiriki kikamilifu
Kwa mujibu wa ratiba ya Uchaguzi huo zoezi la kuchukua fumu litafanyika kuanzia Oktoba 26 mwaka huu.