KOMBO: WANANCHI MSISHIRIKI MAANDAMANO YA CHADEMA


Na Mwandishi Wetu, Dar

Wananchi hususani  vijana wameaswa kutoshiriki maandano ya Chama cha  Demokrasia Na Maendeleo  CHADEMA yanayotarijiwa  septemba 23 jijini Dar es salaam.

 Akizungumza na waandishi wa Habari leo septemba 21,  Mwanaharati Ahamed Kombo  amesema maandamano hayo yana  lengo baya la  kuvurugu amani ya nchi kwa ujumla.

"Nawasihi watanzania wasije  wakashiriki maandamano yao wanaotaka kufanya chadema yana lengo ya kuleta vurugu na kuharibu amani ya nchi"

 Amesema kuwa Wametengeza kundi ambalo lipo kibaha ambalo lina watu 12 ambalo wanapewa mafunzo ya kikomando kwajili ya maandano ya tarehe  23.

Aidha amesema watanzania kuwa Makii  makini  kwa ukiona serikali imezuia maandamano jua kuna jambo la siri limejificha kwa taifa likifanyika linakuwa halina afya.

"Niwaombe sana watanzania kutoshiriki maandamano haya kwa kufikilia familia zenu pamoja na watoto wenu maana chadema hawana nia njema na taifa letu" amesema.

Ameongeza"Watanzania hatuhitaji maandamano watanzania tunahitaji maendeleo na kumsapoti Rais wetu Samia Suluhu Hassan Wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania"

"Ukiona serikali imezuia  maandano ujue kuna jambo baya la siri litaka kufanyika na chama cha Chadema" amesema Mwanaharaki Kombo.

Kwa Upande wake Mwanaharakati Joseph Yona amesema  Chadema wamechukua wakufunzi 12 kutoka kenye kuwapata mafunzo vijana kutoka mikoq mbalimbali namna ya kuandamana

"Miaka ya nyuma ilishawahi kutoka hapa Tanzania yakaua Mdada asiye na hatia Akwelina kwa sababu ya jeuri ya kina Freeman Mbowe" amesema Yona

Amesema chama  Chadema kinatakiwa kutii na  kukubaliana na Jeshi la polisi kwa kuzuia maandamano yao ya tarehe 23.

Ameongeza " Maandamano ya jumatatu mwenyekiti freeman mbowe wameandaa mandamano kwajili ya kwenda kutenda kitu cha ajabu ili jeshi la polisi lichukue maamuzi na mataifa ya nje yawatetee"

Aidha ameliomba jeshi la polisi kuwa makini kwani ikitokea chadema wameandike Free mtu fulani ujue kuna mtu atapozea maisha yake.
Previous Post Next Post