DCP MWAMINI: UCHUNGUZI WA SAYANSI UMEKUWA NA MCHANGO MKUBWA KATIKA KUSAIDIA KUTENDA HAKI


Na lilian Ekonga Dar es Salaam.

Naibu Kamshina wa Polisi  (DCP),Mwamini Rwantale ametoa maelekezo kwa watendaji wa Jeshi la Polisi katika maabara za uchunguzi wa sayansi jinai kuzingatia umahili kwenye shughuli zao ili kuepuka kutiliwa shaka majibu yao.

Amesema majibu na vielelezo vyao vinategemewa kutenda haki kwa jamii na vyombo vya maamuzi ikiwemo mahakama katika kufanya maamuzi ya  kisheria.

Rwantale ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Sayansi asili ndani ya Jeshi hilo amesema ni muhimu kwa wataalamu wa tasnia hiyo kuzingatia maelekezo hayo kwa kuwa jeshi hilo lipo katika awamu ya pili ya maboresho na utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai iliyoundwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza akiwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Uchunguzi wa Kisayansi wa makosa ya Jinai (Forensic Day) ambayo kwa Tanzania ni mara ya kwanza kuadhimishwa amesema itakuwa aibu majibu yao kufanyiwa uchunguzi tena ili kujiridhisha.

"Sayansi imekuwa na mchango mkubwa katika maisha ya binadamu katika kusaidia kutendeka haki, tumeshuhudia wahalifu wakibainika kirahisi.Nawasiokuwa na hatia kuachiwa  kuachiwa huru," amesema 

Katika maelezo yake amesema wakati wakiadhimisha siku hiyo iliyoanzishwa 1955 huko Ubelgiji ni muhimu kwa wataalamu wa tasnia hiyo kuzingatia mchakato huo kwa uadilifu katika maabara zao katika kubaini ukweli.

"Maadhimisho haya yamekuja muda muafaka, jeshi lipo katika maboresho ya awamu ya pili yanayoenda sambamba na utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya haki Jinai yanalenga kubadilisha fikra na kuacha kufanya kazi kwa mazoea," amesema

Naye,Meneja wa Maabara ya Sayansi Jinai kutoka Ofisi kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali,Fidelis Segumba amesema katika utendaji wa shughuli zao huwa wanashirikiana na wadau kama Jeshi la Polisi.

"Ni Muhimu kwa wataalamu wa eneo hili kuzingatia weledi tangu wanapoanza kuchukua sampuli kuzitenganisha vizuri hadi wanakovifikisha ili kuondoa mkanganyiko," amesema 

Awali,Ofisa kutoka Ofisi ya Mdhibiti wa Madawa ya Kulevya nchini,Peter Patrick amesema wameanzisha maabara ya Sayansi jinai katika utambuzi wa madawa mapya yanayozalishwa sehemu mbalimbali na kuingizwa nchini.

"Tatizo hilo ni kubwa na mwaka 2023 kulikuwa na dawa za kulevya mpya zaidi ya 1000 zilizoingizwa sokoni na majina yake ni tofauti zinazotambuliwa katika orodha ya madawa yaliyopo lakini maabara hii imekuwa ikitusaidia kudhibiti kwakuwa tunamitambo ya kisasa," amesema 

Siku ya Sanyansi ya Uchunguzi Duniani huadhimishwa kila ifikapo Septemba 20 kila mwaka ili kuwakumbusha watendaji wa kada hiyo kuzingatia weledi kupitia kazi yao kuisaidia jamii kujua ukweli.
Previous Post Next Post