DART YAZINDUA MFUMO WA MALIPO YA TIKETI KWA KADI


Na Lilian Ekonga. Dar es salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi) Mohamed Mchengerwa amewataka  wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART) na UDART  washirikiane ili kutatua changamoto zinazowakabili wananchi ili kuongeza ufanisi wenye tija kwenye kutoa huduma hiyo .

Hayo ameyasema Leo Septemba 2   Jijini Dar es salaam wakati aa uzinduzi wa mageti janja,kadi janja kwa ajili ya mwendokasi .

Mchengerwa amesema kumekuwa na baadhi ya madereva wa mabasi yaendayo haraka wanatumia kauli sizizofaa kwa abiria hali inayoleta changamoto kwa wananchi wanatumia usafiri huo.

Amesema  mfumo huo wa ukataji tiketi janja Itasaidia kuondoa  udanganyifu kwenye mapato, kuokoa muda , kutunza mazingira ukilinganisha na awali walipokuwa wakitumia tiketi za karatasi  huku akisema dhamira ya serikali ni kutibu hoja za wananchi za mda mrefu

Aidha amesema kutumia kadi janja hizo ni kuendana na teknolojia ya kiwango cha juu na mapinduzi makubwa ya kuwahudumia watanzania wa Mkoa wa Dar es salaam 

Huku  MChengerwa akiwataka wakala wa mabasi hayo kabla ya Disemba mwaka huu Mkoa wa Dar es salaam uwe na mabasi ya kutosha yatakayokidhi huduma za wananchi wa Mkoa huo .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa mabasi yaendayo haraka  (DART)Dk. Othuman Kihamia amesema mfumo wa ukataji tiketi  kwa kutumia kadi janja utasaidia kuondoa matumizi ya katasi na kuchafua mazingira,Usumbufu wa chenchi, pamoja na kupunguza foleni wakati wa ukataji wa tiketi.

Mfumo huo wa kadi janja unaanza kutumika rasmi leo kwenye vituo vyote vya mabasi yaendayo haraka Jijini Dar es salaam.
Previous Post Next Post