CRDB BANK FOUNDATION YAZINDUA KAMPENI YA KUWAUNGANISHA WAJASIRIAMALI WADOGO NA PROGRAM YA IMBEJU


Na Lilian Ekonga

Taasisi ya CRDB Bank Foundation imezindua rasmi kampeni maalum ya IMBEJU inayolenga kuwaunganisha vijana na wanawake wajasiriamali nchini na programu ya IMBEJU. 

Akizungumza na wandishi wa Habari  katika hafla ya uzinduzi Leo Agust 30, Mkurugenzi wa Wateja wadogo  na wakati  wa Benki ya CRDB, Bonaventura Paul amesema kampeni hiyo iliyopewa jina la ‘IMBEJU Uwezeshaji’ ambayo inalenga kuwafikia wajasirimiali wadogo wadogo kote nchini.ususani wale walio maeneo ya pembezoni na vijijini jambo ambalo litasaidia si tu kukuza ujumuishi wa kifedha bali pia kukuza sekta ya ujasiriamali na uchumi wa Taifa kwa ujumla

"Huduma za kifedha zina mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi, na ndio maana Benki ya CRDB imekuwa mstari wa mbele kubuni bidhaa na huduma zinazolenga makundi mbalimbali ya jamii. Tunajivunia kuwa sehemu ya kampeni hii inayoendeshwa na wenzetu wa CRDB Bank Foundation ambayo tunaamini itakwenda kukuza ujumishi kwa wanawake na vijana wengi ambao ndio sehemu kubwa ya wajasiriamali nchini," amesema Bonaventura.

Aidha, Bonaventura amewataka wanawake na vijana wajasiriamali kote nchini kujiunga na programu ya IMBEJU ili kukuza na kuboresha biashara zao huku akieleza kuwa katika matawi yote ya Benki ya CRDB zaidi ya 260 kuna dirisha maalum kwa ajili ya programu hiyo. 

"Malengo yetu ni kuwa baada ya kuhitimu programu hii, wataweza Kuunganishwa na uwezeshaji kupitia Benki yao ya CRDB ambapo kupitia Idara yetu ya Wateja Wadogo na Wakati wataweza kukopeshwa hadi shilingi bilioni 3 kulingana na uwezo wa ulipaji wa biashara zao," aliongeza.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Fadhil Bushagama, ameeleza kuwa kampeni hiyo ya IMBEJU Uwezeshaji ni sehemu ya juhudi za taasisi hiyo katika kukuza ujumuishi wa kifedha na kiuchumi ili kuboresha maisha ya vijana na wanawake wajasiriamali. 

"Programu ya IMBEJU imeleta mapinduzi makubwa katika kuchochea ujumuishi wa kifedha, ambapo zaidi ya wanawake na vijana wajasiriamali 600,000 wamefikiwa na mitaji wezeshi ya zaidi ya shilingi bilioni 11 imetolewa," amesema Bushagama.

Bushagama amesema awamu ya kwanza ya kampeni ya ‘IMBEJU Uwezeshaji’ inatarajiwa kuanzia Kanda ya Nyanda za Juu katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Ruvuma, Njombe, Katavi, na Rukwa ambapo wajasiriamali zaidi ya 12,000 na vikundi vya wajasiriamali 1,000 vinatarajiwa kufikiwa.

“Timu yetu kutoka Makao Makuu kwa kushirikiana na matawi ya Benki yetu ya CRDB katika mikoa hiyo, pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii tutashirikiana kwa pamoja kutoa elimu ya fedha, mafunzo ya biashara na ujasirimali. Baada ya kanda hiyo tutakwenda Kanda ya Kusini na Kanda ya Kati,” aliongezea Bushagama.

Akitoa shukrani kwa washirika wa programu ya IMBEJU, Bushagama ameishukuru Serikali chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka sera na mazingira wezeshi ya uwezeshaji wa vijana na wanawake nchini. Amesema Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Watoto, na Makundi Maaulum pamoja na Wizara ya TAMISEMI imekuwa mshirika wa karibu katika utekelezaji wa programu ya IMBEJU.
Previous Post Next Post