WAZIRI BASHE AMEZITAKA NCHI ZA AFRIKA KUWEKA SERA NZURI KATIKA KILIMO


Na Lilian Ekonga Dar es salaam.

 Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amezitaka nchi za Afrika kuwa na sera nzuri za uwekezaji katika sekta ya kilimo ili kuharakisha maendeleo ya sekta hiyo  na kukuza uchumi wa Afrika.

Akizungumza wakati wa kuzindua mpango mkuu wa maendeleo wa mifumo ya chakula 2030 uliofanyika jijini Dar es Salaam, Waziri Bashe amesema asilimia kubwa ya uzalishaji wa mifumo ya chakula bado hauridhishi kulingana na mahitaji ya chakula katika Bara la Afrika.

Bashe amewataka wadau wa mifumo ya chakula Barani Afrika AGRF kuanza  kuainisha  maeneo  muhimu ya uwekezaji ili kuifanya sekta hiyo kuvutia kwa watu wengi likiwemo kundi la vijana. 

"Mpango huu wa uboreshaji wa mifumo ya chakula 2050 unapaswa  kulingana na maono ya maendeleo ya mwaka na dhamira yake utaonekana  Agosti mwaka  huu hicho ndicho tunachotaka na kielelezo tosha kwa taifa,” amesema  Waziri Bashe.

“Nadhani sasa hadithi na majadiliano ya maendeleo ya kilimo lazima yaingizwe katika mifumo ya chakula lengo ni kutaka kuhamasisha pia kundi la vijana ambalo linahitaji kuwezesha kiteknolojia, fedha na uhakika wa masoko  huo ndio mwelekeo wa serikali “alisisitiza Waziri Bashe

Katika Mahojiano na waandishi Mkutano huo wa waandishi wa habari umehusisha mahojiano na Waziri Mkuu (mstaafu) wa Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya AGRA; Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb); Mtendaji wa Kanda ya Afrika Mashariki wa IFAD, Bi. Sara Mbago-Bhuno; Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Shamata Shaame Khamis (Mb) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Edwin Paul Mhede. 

Masuala mbalimbali yamezungumzwa katika magojiano hayo likiwemo uzinduzi wa kitabu cha dira ya Ajenda 10/30 chenye lengo la  ya uwekezaji kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kukuza kilimo chenye tija nchini Tanzania.  Mkakati wa kitabu hicho pia una shabaha ya kuweka malengo kabambe ya ukuaji wa uchumi kwa muongo ujao ikiwa ni pamoja na kuchochea ukuaji wa kilimo kufikia asimilia 10 ifikapo mwaka 2030.
Previous Post Next Post