Na Lilian Ekonga, Dar es salaam
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Jerald Mweli amewataka vijana kuchangamkia fursa zilizopo katika miradi ya kilimo ili kujitengenezea ajira ya kudumu.
Mweli amesema hayo katika kongamano la vijana wanaojishughulisha na kilimo nchini lililoandaliwa na shirika la mageuzi ya kijana Tanzania(AGRA) kupitia mradi wa Building a Better Tomorrow (BBT)Julai 5,2024 uliohudhuriwa na vijana 100 toka mikoa mbalimbali Nchini.
"Wizara ya kilimo kwa kushirikiana na Asasi zisizo za kiserikali tumeandaa mpango maalumu kuhakikisha vijana wanajitengenezea ajira ya kudumu kupitia kilimo,na sasa hivi International Forum zote zitahusisha vijana ambapo vijana watakuwa wakisafiri nje ya nchi ili wakajifunze namna ya kuwekeza kwenye kilimo,nitoe wito kwa vijana jiajilini kwenye kilimo kilimo kina lipa na sasa hivi baadhi ya mashirika toka mataifa ya nje yanataka kuleta fund kwa ajili ya vijana wa kitanzania wanaojihusisha na kilimo"Amesema Mweli.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa shirika la uboreshajibwa kijana Tanzania (Agra) Vianey Rweyendela amesema kukua kwa uchimi wa Tanzania uliofikia 5.1% kwa mwaka kunatokana na shughuli za kilimo.
"Kukua kwa uchimi w Nchi umetokana na kilimo kwani 65%ya watanzania wanaishi kwa kutegemea kilimo" amesema Rweyendele
Ameongeza kuwa katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan Bajeti ya kilomo imeongezeka zaisi ya mara 5 tofauti na vipindi vilivyopota na kwamba lengo la kuongeza bajeti ni kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kwamba Agra kupitia mradi wa BBT imelenga kusaidia vijana wakulima katika upatikanaji wa Masoko,madhamba na kuwakopesha fedha ili waweze kufanya shuguli za kilimo.
Nae Emmanuel kisinda, mkurugenzi wa Kikomba Avocado farm, amesema wananufaika na AGRA na wapo katika mafunzo hayo kwa lengo la kujua sera za namna gani amabazo wanaweza kuon kijan asaidiwe kwenye upatikanaji wa makoso, pesa na ardhi.
Mkame Tetere ambaye ni mkurugenzi wa Makame limited amesema wao kama wakulima wanachangamoto mbalimbali ambazo wanakutano nazo ikiwemo wa ukosefu wa mbegu kwa walikuma wa vujiji
"Tunaamini AGRA wakiweka mfumo mzuri wa kuwakopesha wakulima mbegu moja kwa moja na ambao hataweza kuwabana wakulima" amesema mkame.