ZAIDI YA MABALOZI 62 KUSHIRIKI AFRIKA MARATHON


Na mwandishi wetu

ZAIDI ya Mabalozi   62 na wanadiplomasia wanatarajia kushiriki mbio za Marathon za kilometa 5 hadi km15 zinazo tarajia kuanza Mei18 Mwaka huu katika Daraja Tanzanate,Mtaa wa Baraka Obama hadi Masaki jijini  Dar es Salaam.


Akizungumza na Waandishi  Habari jijini Dar es  Salaam Mkurugenzi wa idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ally Bujiku amesema kuwa Mbio hizo za Afrika Marathon zinalenga kuadhimisha  miaka 61ya Maadhisho ya Nchi huru za Umoja wa Afrika ambapo lengo mbio hizo ni kukuza Diplomasia katika sekta ya Michezo.



 "Michezo ni Biashara,ni Ajira ni kazi pia ni Diplomasia,Tumechagua Riadha kwasababu kila mtu Anaweza kushiriki"Alisema Mkurugenzi wa Idara  ya Afrika Wizara ya Mambo ya nje Balozi Ally Bujiku.

Balozi Bujiku aliongeza kuwa Sambamba na Mbio hizo pia kutakuwa na Chakula chapamoja  katika Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.

Aidha,Balozi wa Somalia Nchini Tanzania YassiniAlly khali amesema yupo tayari kukimbia kilometa 15 zitakazo anza ukumbi wa Mwalimu Nyerere  hadi Masaki.


kwa upande wa Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Mambo ya nje  Ushirikiano  wa Afrika Mashariki Mindi kasiga  amesema mbio hizo zinatarajiwa kuhudhuriwa wanariadha na kama vile Filbart Bayi Juma ikanga Magedalena.

"Pia shule mbalimbali zinatarajiwa kushiriki  ikiwemo Pugu,Uhuru Mchanganyiko,Pamoja Jangwani sekondari"Amesema  Mkuu wa kitengo cha Mawasilano wizara ya mambo ya nje Mindi kasiga.
Previous Post Next Post