Na Lilian Ekonga, Dar es salaam.
Shirika la Foundation Civil of sociefy (FCS) wamesaini makataba wa mradi na Taasisi ya Trade Mark Afrika kwa miaka mitatu wenye thamani ya bilioni 2.3 kwa lengo la kuongeza ushiriki wa azaki katika kuboresha ulinzi mlaji na kusaidia biashara iwe jumuisha na endelevu.
AKizungumza na waandishi wa habari mei 14, Mkurugenzi wa FCS, Justice Rutenge amesema mradi utasadia sana katika ulinzi wa walaji kwa upande wa haki pamoja na wajibu wa mlaji na wapi kwa kupeleka mapendekezi kwa bidhaa anayoitumia.
"Sisi kama fsc tutaimarishi ushiriki wa asasi za kiraia kwenye maswala ambayo yanahusu ulinzi wa walaji, azaki zitasaidia kuibua, maoni mapendekezo, malalamiko ikhitajika hatua ya kupeleka madai kwa vyombo mbalimbal8 ili yaweze kufanyiwa ufumbuzi na mlaji aweze kulidwa"amesema Rutenge.
Pia amesema mradi huo utasaidia kuongeza ujumuishi na muendelezo kwenye biashara kwq kuongeza fursa za biashara kwa wanawake,vijana na walemavu.
"Mradi utawawezeha wanawake kuchangamkia fursa hasa katika matumizi ya gesi safi ya kupikia ,kuuza majiko ili waweze kujipatia kipato na kusaidia nchi katika kuendana amabadiliko ya tabia ya nchi" amesema
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Trade Mark Africa, Elibariki shammy amesema wameungana na asasi za kwa kirai kwa lengo la serikali iweze kujua mambo gani yabadilishwe ili wananchi waweza kupata bidhaa kwa bei inayo stahili na waweze kujengea uwezo kutoa elimu kwa wajali na kupata bidhaa zilizo salama zaidi
Aidha amesema mradi huo utaweza kuwawesha wanawake,vijana , wenyeulemavu kuona wanawezaje kuwezesha zaidi kuingia kwenye biashara.
"Kujengea uwezo asasi ya kirai kunaweza kuasidia bidhaa za kitanzania kuweza kushindana katika masoko ya nje" amesema