Waziri Mhagama awashukuru PPRA kwa misaada ya Waathirika wa maafa Hanang


Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama ameupongeza
Uongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Mamlaka ya Ununuzi na Udhubuti wa Umma (PPRA) kwa kutambua na kuungana na Serikali katika kuwashika mkono waathirika wa maafa ya Maporomoko ya Tope na Mawe ya Hanang Mkoani Manyara kwa kuchangia  kiasi cha Shilingi Milioni 16.1 ambazo wamekabidhi hii leo tarehe 28 Disemba, 2023 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.



Akizungumza mara baada ya kupokea misaada hiyo Mhe. Mhagama amewashukuru kwa namna walivyochangia fedha hizo huku akiendelea kutoa wito kwa wadau na wananchi kuendelea kuchangia hasa vifaa vinavyoweza kusaidia katika zoezi la kurejesha hali ikiwemo vifaa vya ujenzi


"Kipekee nawashukuru watumishi wote wa PPRA kwa mchango wenu na niwahakikishie utatumika kama ilivyokusudiwa," alisema Mhe. mhagama


Aidha alieleza kuwa kwa sasa Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan  inaendelea na zoezi muhimu la kurejesha hali kwa wana Hanang ili kuwapa maisha yenye ubora na furaha na kuhakikisha Watanzania wenzetu wanaendelea na shughuli zao za kujiletea maendeleo kama ilivyopaswa kuwa.


Previous Post Next Post