Mwenyekiti wa UWT Babati Mjini atumia kumbukizi ya kuzaliwa kugawa taulo za kike kwa wanafunzi


Na Mary Margwe, Babati

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Babati Mjini Mkoani Manyara Eva Makilagi Luoga  ameitumia siku ya kumbukizi au  mfanano ya siku yake ya kuzaliwa ( Birthday ) kwenda kuwatembelea watoto yatima na Wanafunzi na kutoa msaada.


Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Mfanyabiashara wa Saloon na Nguo za Maharusi Mjini Babati kila mwaka ifikapo Mwezi Novemba 10 husheherekia siku ya mfanano wa kuzaliwa kwake ambapo akitembelea shule ya Sekondari Kwaang'w na kutoa taulo za kike 150 Kwa wanafunzi wa kidato cha nne.


" Nimeona nije niwatembelee watoto wangu, wanafunzi wetu kuwatia Moyo katika mitihani yenu ya kidato cha nne, naomba mtulie muweze kuifanya vema mitihani yenu, Si mnaona Rais wetu Samia Suluhu Hassan ni Mawanamke na anataja wanafunzi wasome kwa bidii ili kufikia malengo tmliyoyakusudia, hivyo nimewaletea taulo za kike  150 mtazipokea ninyi mkiwaakilisha wenzenu wote" amesema Luoga.


Mbali kuwatembelea wanafunzi hao pia alitumia siku hiyo kuwatembelea watoto yatima wanaolelewa katika kituo Cha kulelea watoto Hosasana kilichopo Kata ya Singe, ambapo alifanikiwa kuwapekea sabuni ya unga pamoja na juisi.
Previous Post Next Post