Kampuni ya Franone Mining, Madini ya Tanzanite ni kivutio kikubwa Maonyesho ya Madini Geita, Serikali yaipongeza



Na Humphrey Msechu, Geita

Naingia katika Banda la Tume ya Madini, kushoto kwangu nakutana na madini mazuri, yenye mvuto wa rangi ya blue inayobadilika badilika kwa kadri unavyoyashika nayo hubadilika kulingana na utakavyoyaweka aamkuyageuza geuza mkononi mwako.

Pembeni namuona Binti mrembo kabisa aliyejitambulisha Kwa jina la Furaha Mshai namuuliza ananijibu kuwa yeye ni mfanyakazi kutoka Kampuni ya Franone Mining, yupo vizuri, kuwahudumia na kutoa elimu ya Madini pendwa duniani ya Tanzanite ambapo watu mbalimbali kutoka nchini Kenya, Malawi, Zambia, DRC Congo, Uganda, Rwanda, na Burundi, walifurika kujionea kwa macho Madini ya Tanzanite.

Watanzania nao hawakua mbali Wenda kuzungukia Banda la Franone Mining ( mithili ya nyuki katika mzinga wake wa asali, ama hakika ina furahisha kweli kweli , wanafunzi nao walikua hawabanduki katika banda hilo ili mladi tu nao waweze kuyaona Madini ya Tanzanite na hatimaye waweze kwenda kuwasimulia walichokiona ndani ya banda la Franone Mining.

Hakika Banda la Franone Mining ni Banda lililokua na mvuto mkubwa na wa aina yake katika Maonyesho ya 6 ya Kimataifa na Teknolojia ya Madini yaliyofanyika katika Viwanja vya Bombambili Halmashauri ya Mji wa Geita.

Kampuni ya Franone Mining and Gems Ltd inayojihusisha na uchimbaji wa kati wa madini ya Tanzanite katika Kitalu C nanD inayomilikiwa na mwekezaji mzawa Onesmo Anderson Mbise, Francis Matunda, imekua ni kivutio kikubwa katika Maonyesho hayo Mjini Geita.


Katika Maonyesho hayo Kampuni ya Franone Mining ilikua ndani ya banda la Tume ya Madini, hivyo kila kiongozi na baadhi ya Wananchi wa Kanda ya ziwa kwao kulikua ni kivutio kikubwa kuiona Kampuni ya Franone Mining inayozalisha Madini ya Tanzanite ambapo hupatikani Mkoani Manyara Wilaya ya Simanjiro Kata ya Naisinyai na Mirerani pekee duniani.

Upekee wa Madini ya Tanzanite yaliwafanya watu kutoka Mikoa mbalimbali ndani na nje ya nchi kuweza kutembelea Banda la Franone ili tu waweze kuyaona kama sio kuyashika kabisa lakini hata kuyaona kwa macho.

 Jamii mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa shule mbaliiiii za Sekondari ndani ya mkoa na nje ya Mkoa huo walifikankatika Banda hilo nankufanya utalii wa ndani ili kujionea Madini ya Tanzanite.

*NENO KWA MBUNGE WA GEITA MJINI MH. KANYASU

Hapa Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu anatumia nafasi yake kuipongeza Kampuni ya Franone Mining kwa kuleta Madini ya kipekee, Madini pendwa ya Tanzanite ambayo hupatikana katika Mji Mdogo wa Mirerani duniani kote.

" Binafsi nimefurahi sana kuyaona Madini ya Tanzanite katika Maonyesho haya, Franone Mining mmefanya vizuri sana kuja na kushiriki pamoja nasi katika Maonyesho haya ya sita ya Kimataifa na Teknolojia ya Madini Geita, hivyo Franone mmefanya vizuri kuja na Madini ya Tanzanite ili kila Mtanzania nanwa nchi nyingine waweze kuyaona Moja kwa Moja.

Aidha hapa Mbunge Kanyasu anaiomba Wizara ya madini kuhakikisha kipindi kijavho wanaandaa Banda maalumkwa ajili ya kuuzia bidhaa ya Tanzanite na ukilinganisha na Dar es Salaam wakati wa Maonyesho kulikua na bidhaa mbalimbali kama heleni, cheni, na vingine vingi.

*NENO KWA WAZIRI WA MADINI MH.MAVUNDE

Waziri wa Madini Anthony Mavunde naye anapata fursa ya kutembelea mabanda, na hapa anaingia katika Banda la Tume ya Madini na kukutana na kampuni ya Franone Mining wanaochimba Madini ya Tanzanite.

" Kupitia Maonyesho haya Watanzania wamepata nafasi ya kujifunza, na kuona Teknolojia mbalimbali, lakini pia kubadilisha uzoefu na watu, wataalamu kutoka maeneo mbalimbali na hivyo Maonyesho haya yamekua na tija kubwa sana, sisi kama Wizara ya madini tutaendelea kuwaunga mkono kuhakikisha tunaonyesha Mwaka hadi Mwaka na kuongeza ubora wake" anasema Mavunde.


Wachimbaji wadogo nchini wasijione wanyonge ila wachangamkie fursa za uchimbaji, ambapo Serikali imeweka mazingira mazuri na mikakati bora kabisa katika kuwainua kiuchumi wachimbaji nchini,ambapo anasema baada ya mpango wa Building a Better Tomorrow (BBT) kufanikiwa katika Wizara ya Kilimo wapo mbioni kuanzisha mpango wa uchimbaji kwa maisha bora ya baadaye, Mining for a Brighter Tomorrow (MBT) kwenye Wizara ya Madini.
“Wachimbaji wadogo msiwe wanyonge, tuna mpango wa kuwawezesha ili uchimbaji wenu uwe na tija kupitia dira ya 2030 madini ni maisha na utajiri,” amesema Waziri Mavunde
Aidha anafafanua kuwa dhamira ya Wizara ya Madini kuona maonyeaho haya yanakua ni Maonyesho makubwa sana katika ukanda wa Afrika Mashariki na kama sio Afrika nzima, na hiyo ndio dhamira ya Wizara ya Madini.

Hapa Waziri Mavunde anatumia fursa hiyo kuwataka wadau mbalimbali wa Madini kuyatumia Maonyesho haya kama sehemu ya kutoa elimu ,lakini vile vile kama sehemu ya kuongeza uzoefu na kujifunza kwa wadau mbalimbali walioko hapo.


Akizungumza kwenye mahojiano maalum na chombo hiki Meneja Mkuu wa Mgodi wa Kampuni ya Franone Mining Visema kuwa kampuni hiyo iliyoanza tangu mwaka 2011 imekuwa na rekodi ya kutoka katika uchimbaji mdogo hadi kufikia uchimbaji wa kati.
Ndakize anatumia fursa yake akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari kwenye maonesho hayo na huku akiishukuru Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini kwa miongozo na maelekezo kwa wachimbaji wadogo kupiga hatua kutoka uchimbaji mdogo na kuwa wachimbaji wa kati na hatimaye kuwa mchimbaji mkubwa.

" Kutokana na jitihada za Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluh Hassan alizozifanya kwenye Sekta ya Madini tumeweza kuinuka wachimbaji kutoka uchimbaji mdogo hadi kufikia uchimbaji wa kati, hivyo tunamshukuru sana mama yetu, Rais wetu Dk.Samia Suluhu Hassan" anasema Ndakize

Akieleza mipango ya Kampuni amesema kuwa wamejiwekea kukua zaidi na kutengeneza ajira nyingi kwa Watanzania pamoja na kuendelea kuongeza migodi katika Mikoa mingine, ambapo anaongeza kuwa wana Ofisi katika Mkoa wa Manyara na Morogoro .

Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya Franone Mining LTD, Napokye Baraka Kanunga amemuonyesha Waziri Mavunde madini ya Tanzanite na kusema yana rangi ya mvuto wa blue na yanabadilika rangi pindi ukiyashika na kuyageuza.

“Kampuni ya Franone Mining and Gems LTD ndiyo inayomiliki machimbo ya madini ya Tanzanite kwenye kitalu C mji mdogo wa Mirerani na tumekuja kushiriki maonyesho haya ili kuwaonyesha wakazi wa kanda ya ziwa madini ya Tanzanite,” amesema Napokye.

Mchimbaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani, Fatuma Kikuyu amemueleza Waziri Mavunde, kuwawezesha wachimbaji wadogo ili wawe makampuni makubwa kama ya GGM LTD ya dhahabu na Franone Mining LTD ya Tanzanite.

Mmoja kati ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Nyankumbu Girls Aneth ya Mjini Geita Sulle amesema " Mimi Madini ya Tanzanite Huwa nayasikia tu kwenye redio namkuyaonankwenye Tv, hivyo kupitia Maonyesho haya nashukuru sana Leo nimeweza kuyaona kwa macho yangu, hakika nimefurahi sana maana kila mmoja alikua anagombania kupata nafasi ya kuyaona Madini ya Tanzanite" anasema Sulle.

Haya hivyo Aneth Sulle ameipongeza Kampuni ya Franone Mining chininyanuongozi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Onesmo Anderson Mbise kwa kutoa wafanyakazi wake kuja kwenye Maonyesho haya ambapo imesaidia watu wengi kuyaona , kwani wapo wanaotoka nchi mbalimbali kwenda Manyara Mirerani Kwa lengo tu la kwenda kuyaona Madini ya Tanzanite.
Previous Post Next Post