JERRY SILAHA ATOA SIKU SABA KWA WATENDAJI WA WIZARA YA ARDHI


Na Mwandishi wetu

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaha amewataka Watendaji wa Ardhi kuwachukulia Hatua Makampuni yanayohusisha na urasimishaji wa Ardhi yalikiuka Sheria za urasmishaji wa Ardhi kwa kipindi cha siku saba.

Akizungumza katika kikao cha Chama cha Mapinduzi wa Mkoa wa Dar es salaam Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaha amesema lengo la Serikali nikupanua wigo wa huduma za Ardhi kwa wananchi.

"Ni vyema tukaweka mikakati ya kutatua tatizo hili moja wapo nikuwa namikoa maalumu ya kiardhi ilikutatua changamoto ya Ardhi katika Mkoa wa Dar es Salaam"Alisema Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Jerry Silaha .

Silaha alisema kuwa ilani ya chama cha Mapinduzi imetoa ahadi kwa wananchi kuwa watapimiwa Ardhi zoezi hilo linaendana sambamba na utoaji hati zaidi ya milionmoja kwa wakaazi wa Dar es salaam.

Alisema kuwa Hatua zinazo kwamisha zoezi hilo nikutokana na uhaba wa watumishi na vifaa pamoja Rasmali fedha ni Moja ya Changamoto zinazokwamisha zoezi la urasimishaji wa Ardhi.

Naye Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam wa  Chama Cha Mapinduzi Abbass Mtevu amesema kutokana nakuwepo kwa changamoto nyingi katika sekta ya Ardhi wamemuomba waziri huyo kuweza kutafuta ufumbuzi wa kero za urasimishaji wa Ardhi.

"Kumekuwa na Makampuni  yamekuwa yakirasmisha Ardhi halafu yanapotea hasa kata kisukulu".AlisemaMwenyekiti Abbas Mtevu.

Mtevu alisema jiji la Dar es salaam lina kata 102 lakini kumekuwa na kero za Ardhi na kumuomba waziri huyo  aliyepewa dhamana ya Ardhi kutatua changamoto hizo.
Previous Post Next Post