TCCA YABORESHA MFUMO WA UTAOAJI TAARIFA ZA KIANGA


Na Lilian Ekonga

Mamlaka ya Usafari Anga Tanzania(TCAA) wamesaini mkataba wa mradi na Kampuni ya Indra Avitech utakohusika kutengeneza Mfumo wa upatashanaji na ubadilishaji wa taarifa za kianga wenye lengo la kuwa na Kanzi Data itakayosaidia kuhakikisha taraifa zote za kianga zinatolewa kwa ubora, kwa wakati na ufanisi mkubwa kwa watuamiaji wa Anga la Tanzania. 

Akizungumz na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaa, Mkurugenzi wa TCAA ,Hamza Johari Amesema Mkataba huo unathamani ya shilingi Bilioni 9 za kitanzania na utatekelezwa kwa muda miezi 18.


"Lazima tuwe na Kanzi Data ama utaratibu mzuri wa kubadilishana taarifa za kianga kwa ubora na kwa wakati na kuachana na utaribu tuona utumia sasa wa kutoa taarifa kwa kuandika kwenye Mbao ambapo inaathiri kwa wengine kutoweza kupata taarifa kwa wakati" amesema Johari


Pia amesena Anga la Tanzania litapokuwa na huduma bora itachangia kuongezeka kwa wingi wa ndege nchini zitakazowezesha kuchangia kukua kwa biashara ambazo zitaweza kufanyika na kupelekea kukua kwa uchimi. 

Ameongeza kuwa katika kuhakikisha wanaboresha shughuli nzima za kianga walihakikisha kwamba mifumo yote ya kianga inakuwa mizuri kwa kila kinachoruka angani kinaweza kuonwa ili kuweza kusimamia Anga vizuri.

Aidha amesema wameweza kufanya mradi wa sauti katika kuboresha huduma ya mawasiliano kupitia radio kwa mabaruni wanaoruka na ndege na watu wa wanaongoza ndege.

"Nchi nyingine ambazo zimechukua mradi kama huu ni Mamlaka ya usafiri wa Anga wa Kenya, Uganda, Dubai, Ujerumani na Eswatini"amesema.
Previous Post Next Post