TAASISI YA MOYO YA JAKAYA ( JKCI ) YALETA KLINIKI MAALUM "V.I.P CLINIC" KWENYE MAONYESHO YA MADINI, GEITA


Na Mwanahabari wetu,Geita

TAASISI ya Moyo ya Jakaya  Kikwete (JKCI) imeleta kliniki ya maalum"V.I.P" ya huduma ya magonjwa ya moyo,Kliniki hiyo maalum inapatikana katika  maonyesho ya sita(6) ya madini yanayofanyika kuanzia tarehe 20 september mpaka 30 September mwaka katika viwanja vya Bombambili mkoani Geita.

Akizungumza na waandishi wa habari Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo Dr.Salehe Mwinchete alisema "leo tumeleta katikq maonyesho ya madini hii kliniki maalum inaitwa V.I.P Clinic ambayo ni kliniki ya watu mashauri lakini kwetu sio watu mashauri wenye pesa hii kliniki ni kwa kila mtu mwenye uhitaji wa huduma hii"


Aidha,Dkt Salehe amefafanua jinsi kliniki hiyo inavyotoa huduma alisema "Mtu ataomba siku na muda  ambayo anataka kuja kuhudumiwa katika kliniki maalum, atukutana na mazingira mazuri ya huduma,atafanyiwa huduma zote hapo hapo alipo kwa maana atamuona daktari hapo hapo,atapata vipimo hapo hapo na pia atapatiwa kiburudisho cha chai akiwa anasubiria majibu"


Pia Dkt Salehe ameelezea vyanzo tofauti tofauti vya maradhi ya moyo alisema  kuwa ni ulevi,uvutaji wa sigara,matumizi ya chumvi nyingi katika chakula hivyo ameitaka na kuhihasa jamii kupunguza matumizi ya sigara na pombe ili kuepukana na maradhi ya moyo.

.
Previous Post Next Post