NSSF yajivunia kuongeza thamani ya Mfuko


 Na Humphrey Msechu,Geita

MURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Masha Mshomba amesema ,katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweza kuongeza thamani ya Mfuko huo kutoka Trilioni 4.8 Hadi kufikia shilingi Trilioni 7.6 kwa hesabu zinazoendelea kukaguliwa Hadi hivi sasa.
Mkurugenzi huyo ameyasema hayo mbele ya Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Dkt.Dotyo Biteko alipotembelea Banda hilo ambapo aliipongeza NSSF kwa hatua hiyo.



Masha amesema kuongeza thamani ya Mfuko Hadi kufikia kiasi Cha shilingi Trilioni 7.6 ni hatua kubwa .
"Thamani ya Mfuko imeendelea kukua kwa kasi tukizungumzia mahesabu yaliyokaguliwa  hadi mwaka jana Juni,tuliuwa na mahesabu ya shilingi trilioni 6.08,lakini kwa mwaka huu mpaka kufikia mwezi Juni mwaka huu hesabu ambazo bado zinaendeea kukaguliwa thamani ya Mfuko ni shiingi triioni  7.6"amesema na kuongeza kuwa
“Ni ukuaji mkubwa sana hasa ukizingatia kwamba kabla Rais Samia hajaingia madarakani thamani ya mfuko ilikuwa ni shiingi triioni 4.8 tu."

Akizungumza kuhusu uwepo wao katika maonesho ya Madini amesema wapo kwa sababu ya kuelimisha wadau na wananchi kwa ujumla ilinwaweze kujiunga na Mfuko huo Ili kuendelea kuongeza wananchi na thamani ya Mfuko.



"Katika maonesho hayo tumekuwa na mafanikio makubwa ,tumeongeza wachangiaji wa NSSF ambapo kwa mkoa wa Geita tunakusanya shilingi bilioni 96 ,lakini wakati Rais Samia anaingia madarakani kwa mkoa huu tulikuwa tunapokea michango ya shilingi bilioni 26 tu,tunaamini tutaendelea kufanya vizuri zaidi katika miaka ijayo."amesema 


Aidha ameongezea kuwa Mfuko kwa ujumla tumeuwa pia na 'perfomance' nzuri sana ambapo mwaka unaoishia Juni 2023 thamani ya  michango ilikuwa shilingi Trilioni 1.66 na shilingi Trilioni 1.48 kwa mwaka ulioishia Juni 2022 .


Previous Post Next Post