Mbunge Kanyasu awapongeza BRELA kwa kuendelea kutoa elimu kwa Wananchi

Mkuu wa Sehemu ya Majina ya Biashara (Brela) Bw. Harvey Godwin Kombe akimueleza majukumu ya Brela Mbunge wa Jimbo la Geita Mheshimiwa Constantine Kanyasu mara baada ya kutembelea banda lao katika Maonesho ya Sita ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya EPZA Halmashauri ya Mji wa Geita Leo Septemba 26, 2023.


Mkuu wa Sehemu ya Majina ya Biashara (Brela) Bw. Harvey Godwin Kombe akiendelea kutoa Elimu kwa wateja mbalimbali wanaotembelea banda lao katika Maonesho ya Sita ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya EPZA Halmashauri ya Mji wa Geita Leo Septemba 26, 2023.


Mkuu wa Sehemu ya Majina ya Biashara (Brela) Bw. Harvey Godwin Kombe wa kwanza kutoka kushoto, Afisa Leseni wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Jubilate Muro ( katikati) Afisa Usajili Bi. Neema Nyadzi wakiwa tayari kutoa huduma kwa wateja mbalimbali wanaotembelea banda lao katika Maonesho ya Sita ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya EPZA Halmashauri ya Mji wa Geita Leo Septemba 26, 2023.


Na Mwandishi Wetu, Geita


MBUNGE wa Jimbo la Geita Mheshimiwa Constantine Kanyasu amewapongeza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kuendelea kutoa Elimu kwa wadau na wananchi mbalimbali ambao wamekuwa wakitembelea kwenye banda lao kwa lengo la kujua majukumu ya taasisi hiyo.

Ameyasema hayo leo Septemba 26, 2023 Mkoani Geita Mbunge wa Jimbo la Geita Mheshimiwa Constantine Kanyasu mara baada ya kutembelea kwenye banda la Brela lililopo kwenye Maonesho ya Sita ya Madini yanayoendelea katika viwanja vya EPZA Halmashauri ya Mji wa Geita.

Previous Post Next Post