CP KAGANDA AREJEA NCHINI ATAJA MIKAKATI MADHUBUTI KUBORESHA UTENDAJI KAZI KWA ASKARI WAKIKE



Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi- Dar es salaam.

Kamishna wa Polisi Utawala menejimenti ya rasilimali watu CP Suzan Kaganda amerejea nchini na wajumbe aliokuwa ameongozana nao katika Mkutano wa mwaka 2023 wa shirikisho la Jumuiya ya Polisi wanawake Duniani (IAWP) uliofanyika katika mji wa Auckland New Zealand kuanzia Septemba 17 hadi 21,2023.

CP Kaganda amesema lengo la Mkutano huo ni kuwajengea uwezo na kupata mafunzo askari wakike ili waweze kufanya kazi kwa weledi na kutoa huduma bora na nzuri kwa wananchi ambao wanategemea huduma kutoka kwa Jeshi hilo ambalo lina dhamana ya kuwalinda raia na mali zao.

Vilevile Kamishna Kaganda ameongeza kuwa lengo mahususi katika Mkutano huo ni nikuongeza mtandao, mashirikiano na mataifa mengine ya Ulaya na Afrika ili kubadilishana uzoefu katika utendaji wa kazi huku akimshukuru Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyo wawezesha askari wakike kushiriki mikutano mikubwa ya ndani nan je ya nchi ambayo imeleta matokeo Chanya ya kiutendaji.

Sambamba na hilo amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura kwa namna anavyowahamasisha katika ushiriki wa mikutano ya Jumuiya ya Polisi wanawake duniani (IAWP) ambapo ameamtaka Kuwafundisha askari wakike mambo waliojifunza katika mkutano wao uliofanyika Auckland New Zealand.

Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Ilala Kamshna msaidizi wa Polisi ACP Debora Magiligimba ambaye ni mjumbe kutoka Tanzania aliyechaguliwa kuongoza kanda ishirini na moja za nchi za SADC amesema mikutano hiyo ambayo inafanyika kimataifa na kikanda imelenga kuwajengea uwezo askari wa kike duniani huku akibainisha kuwa askari wakike walioshiriki katika Mkutano wa mwezi Julai uliofanyika hapa nchini umewajenga na kuonyesha mabadiliko makubwa ya kiutendaji kutokana na mafunzo hayo.
Previous Post Next Post