TRA YAWATAKA WANANCHI KUWEKA JUHUDI KATIKA ULIPAJI KODI

Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Ndani kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, Ndositwe Haonga akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea Banda la TRA katika maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba).


Salim Bakari Afisa wa Kodi Mwandamizi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Ndani kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, Ndositwe Haonga wakati alipotembelea Banda la TRA katika maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), wa pili kutokakulia ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo.

Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Ndani kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, Ndositwe Haonga katikati akijadiliana jambo na Nasoro Siriwa Mtakwimu Mkuu Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA wakati alipotembelea Banda la TRA katika maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo.


Na Mwandishi Wetu

Watanzania wametakiwa na kuwa juhudi katika kulipa kodi kwani kodi inayolipwa ndio inapelekea serikali kuendeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo elimu, afya na Barabara.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa idara ya mambo ya ndani kutoka Mamlaka ya mapato Tanzania, Ndositwe Haonga wakati alipotembelea Banda la TRA katika maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba).

“Serikali yetu chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni serikali ambayo kwa sasa imejikita sana katika kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo miundombinu kwa kuboresha barabara, uboreshwaji wa shule, maji afya n.k na vyote hivi vinatokana na Kodi ambayo tunaikusanya”

“Wito kwa wadau wetu mbalimbali na wananchi kwa ujumla kuhakikisha kwamba tunalipa Kodi kama ambavyo kaulimbiu yetu inavyosema ukiuza toa risiti na ukinunua dai risiti” Amesema

Haonga alisema wataendeleza elimu ya kulipa Kodi kupitia Vilabu vya kodi katika ngazi ya chini kabisa kuhakikisha kwamba watoto wanakua wakiwa wanajua umuhimu wa kulipa Kodi.

“Tunavyo Vilabu vya Kodi tunataka tupeleke elimu hii kwa watoto wetu wa shule ili elimu ianzie katika ngazi ya chini kabisa kuhakikisha kwamba watoto wetu wanakua wanajua umuhimu wa kulipa Kodi wakiwa bado wadogo ili wanapokua iwe ni rahisi kwao kuweza kuzingatia masuala ya Kodi kuhakikisha na wao wenyewe wanakua na uelewa huo wa Kodi”

Kadhalika Haonga amesema katika Banda la TRA wanatoa huduma mbalimbali kwa wananchi na wadau ambao wanafika kwaajili ya kupata huduma ikiwemo misamaha ya Kodi na kutoa elimu juu ya umuhimu wa kutoa Kodi.

“Tunazo huduma mbalimbali ikiwemo misamaha ya Kodi, kwa mtu yoyote au taasisi yoyote ambayo inawesa ikawa na shida au na mahitaji hayo kutaka kujua ni namna gani zinapatikana na ni jinsi gani ziweze kufanyika au hatua gani afate”

“Tumekuja hapa kutoa elimu juu ya umuhimu wa kutoa Kodi na kuhimiza kwa mfano wengi wetu tunajua kwamba Kodi yetu hii tunayoitoa ndiyo Kodi hiyo hiyo inayotumika kwenye huduma za kijamii kama vile elimu, afya , maji, miundombinu mbalimbali ambayo tunaifanya”

Mbali na hayo, Haonga amesema wanalo pia dawati ambalo linasimamia masuala mazima ya maadili ndani ya Mamlaka ya mapato hivyo amewataka wananchi wote kuripoti masuala yote ya kimaadili ambayo wanakutana nayo.
Previous Post Next Post