TANESCO YAINGIZA FAIDA YA SHILLINGI BILIONI 109

Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba (wapili kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Maharage Chande (wa kwanza kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO Bw. Omari Issa (wa pili kutoka kulia), Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu katika uzinduzi wa taarifa ya mwaka ya fedha 2021/22 pamoja Mpango kazi wa TANESCO miaka 10 iliyofanyika leo tarehe 31/7/2023 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba akizungumza jambo katika uzinduzi wa taarifa ya mwaka ya fedha 2021/22 pamoja Mpango kazi wa TANESCO miaka 10 iliyofanyika leo tarehe 31/7/2023 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya viongozi serikali,Wakuu wa Taasisi mbalimbali pamoja na Wabunge wakiwa katika uzinduzi wa taarifa ya mwaka ya fedha 2021/22 pamoja Mpango kazi wa TANESCO miaka 10 iliyofanyika leo tarehe 31/7/2023 Mlimani City Jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu, Dar

Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba amelipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kufanikiwa kujiendesha kwa mafanikio na kupata faida ya shillingi bilioni 109 katika mwaka 2021/2022 pamoja na kupunguza upotevu wa umeme.

Akizungumza leo tarehe 31/7/2023 jijini Dar es Salaam wakati TANESCO wakizindua ripoti ya mwaka 2021/2022 pamoja na mpango mkakati wa miaka 10 ijayo, Waziri Mhe. Makamba, amesema kuwa TANESCO ni taasisi kubwa hivyo lazima wafanye mabadiliko katika utendaji wao ili kuleta ufanisi wa kisasa wenye kuleta tija.

Mhe. Makamba amesema kuwa serikali itaendelea kutafuta fedha ili tanesco iweze kutimiza majukumu yake katika utekelezaji wa miradi.

Amesema kuwa tanesco inadhamana kubwa katika maendeleo ya nchi katika kuhakikisha malengo tarajiwa yanafikiwa katika nyanja mbalimbali.

“Safari bado ni kubwa, siku zote ili ufanikiwe lazima uwe na mipango kwa ajili ya utekelezaji wenye kuleta tija na mabadiliko ya mafanikio kwa ajili ya watanzania” amesema Mhe. Makamba.

Mhe. Makamba amesema kuwa faida iliyopatikana tanesco ni historia ambayo haijawai kutokea katika Taifa la Tanzania.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Bw. Omari Issa, amesema kuwa wanaendelea kutekeleza majukumu yao ikiwemo kusimamia miradi.

Amesema kuwa ili kuhakikisha tanesco wanafanya vizuri wanaendelea kuwandaa vijana watakaloliongoza Shirika kwa ufanisi.

“Tunakushuru Waziri kwa ushirikiano wako pamoja na wadau mbalimbali tuonaendelea kushirikiana katika kuleta mafanikio Taifa letu” amesema Bw. Issa.

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bw. Maharage Chande, amesema kuwa Shirika limeweka mipango ambayo inakwenda kuleta mabadiliko yenye kuleta manufaa kwa Taifa.

Bw. Chande amesema kuwa katika kipindi cha mwaka 2021/22 wamefanikwa kupata shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi pamoja na wateja wapya 504, 366.

Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu, amezitaka taasisi zote za umma kukabadilika na kuongeza ufanisi katika utendaji pamoja na kuweka wazi, mipango na utekelezaji kwa wananchi.

“Kila taasisi itoe taarifa kwa wananchi ili ijue wanafanya nini katika utekelezaji wa majukumu yao” amesema Bw. Mchechu.

Previous Post Next Post