NABII MKUU DKT. GEORDAVIE APEWA TUZO YA HESHIMA



Na Humphrey Msechu, sparklight tv ARUSHA

WAUMINI wa kanisa la Ngurumo ya Upako wamemtunuku tuzo ya heshima Mheshimiwa Nabii Mkuu Dkt. Geordavie kwa kuthamini na kutambua mchango wake mkubwa wa huduma ya kiroho ambayo imekuwa mkombozi kwa baadhi ya Watanzania Nchini.

Kadinali wa pili wa kanisa la Ngurumo ya Upako ambalo lipo chini ya Nabii Mkuu Dkt GeorDavie, Elizaberth Humphrey kwaniaba ya waumini wa kanisa hilo amesema tuzo hiyo ya heshima ni kutambua kazi kubwa ya kiroho ambayo anaifanya.


Ameyasema hayo Mei 28, 2023 jijini Arusha Kadinali Elizabeth Humphrey kanisani hapo kwenye ibada ambayo iliongozwa na Nabii Mkuu Dkt. Geordavie ambaye siku chache zilizopita alikuwa nchini Afrika Kusini.

Amesema kuwa Nabii Mkuu Dkt Geo Davie amekuwa baraka kubwa Kwa watanzania wakiwamo waumini wa kanisa hilo, Kwa nyakati tofauti amekuwa baraka kubwa Kwa watu mbalimbali na ndio maana wameamua kumpa tuzo hiyo ya heshima.


Ameongeza kuwa tuzo hiyo imetengenezwa china kwa ubora wa hali ya juu sana kama mnavyoona muonekano wake ndani yake ina moyo wa dhahabu safi pia ina ishara ya tufe maana yake dunia nzima inatambua umuhimu wake na gharama yake imeharimu kiasi cha fedha za kitanzania shilingi milioni 10

kwa upande wake balozi wa kanisa hilo Sekela Ntondolo amesema siku imekuwa nzuri sana kwao kwa sababu walikuwa wanamkabidhi baba yao wa kiroho Nabiii mkuu Dkt Geordavie tuzo ya heshima 


"kutambua umuhimu wake hivyo wasingeweza kuona anapewa tuzo na watu wengine ambapo wao wamejisikia fahari sana kwakuonyesha kwamba Nabiii mkuu Dkt Geordavie anafanya kazi kubwa anayoifanya kwenye maisha yao". amesema Sekela

Ameongeza kuwa wengi walifika hapo wakiwa wamefungwa kichumi na nguvu za giza, maisha ni mabaya na hukuna tumaini mahali popote lakini zaidi ya hilo walifunguliwa katika vifungo hivyo napia amewabariki.


Hivyo, Nabii mkuu amekuwa ni mtumishi wa tofauti kabisa na ameleta sura mpya kwa kanisa la Tanzania kwa kupitia hilo ndilo lililopelekea na sisi kutambua kazi yake na kuweza kumpa tuzo ya heshima tunasikia furaha sana kupokea tuzo yetu.
Previous Post Next Post