SERIKALI KUNDAA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA ATHARI ZA MOSHI WA KUPIKIA UTOKANAO NA KUNI



Na Lilian Ekonga, jijini Dar es salaam

Serikali kupitia wizara ya Nishati imeandaa mikakati na  jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa inaokoa maisha na afya za watanzania hususani wa vijijini kutokana na athari za moshi wa kupikia utokanao na kuni.

Hayo ameyasema  Waziri wa Nishati, January Makamba Jijini Dar es Salaam katika siku ya pili ya mjadala wa nishati safi ya kupikia ambapo amesema bajeti ijayo, Serikali itatenga fedha za kutosha zitakazoanzisha mfuko wa nishati safi ya kupikia lengo ni kwenda kumtua mama mzigo wa kuni kichwani.

Waziri amesema utekelezaji wa agizo la Rais la kuunda kikundi kazi cha kitaifa kitakachoratibu dira na mwenendo wa kitaifa wa kuchakata sera na kuleta matokeo chanya ya kuwa na asilimia 90 ya Watanzania watakaokuwa wakitumia Nishati safi ya kupikia katika kipindi cha miaka 10 ijayo kitasaidia kuondoa changamoto wanazopitia watoto na kina mama wa vijijini wakati wa zoezi la kupika




"Sehemu kubwa ya jamii nchini hasa maeneo ya Vijijini imekuwa ikikata miti kwa ajili ya kuni kutokana na bei ya mkaa kuwa chini na hivyo kuhimiza upandaji wa miti ya matunda ambayo wengi wao hawatoweza kuikata bila sababu ya msingi na kwafanya watumie nishati ya gesi kupikia,"amesema waziri Makamba

Ameongeza kuwa  kongamano hilo litasaidia kuokoa maelefu ya Watanzania ambao wamekuwa wakiathirika kutokana na kutumia nishati inayotokana na kuni, mkaa na mabaki ya mazao na vinyesi vya wanyama.

Kwa upande wake Muwakilishi wa Jumuiya ya Umoja wa mataifa inayoshughulikia Maendeleo (UNIDO) Victor Akimu amesema Nishati Safi itasaidia kutunza Mazingira na kukuza uchumi wa nchi.

“Nishati Safi nifursa kwa nchi nahata Dunia ambapo kwa kadri watu wanavyotumia ndipo inajulikana”. Amesema Victor Akimu

Akimu Amesema  Nishati aina Bio Ethano imekuwa ikitumika nchi nyingi ikiwemo Brazil ikifuatiwa na nchi ya Marekani.

Takwimu zinaonyesha kuwa, zaidi ya watu 30,000 wanapoteza maisha kila mwaka kutokana na kutumia nishati ya kuni na mkaa ambayo, kiafya sio salama lakini kutokana na changamoto mbalimbali imewalazimu kutumia.
Previous Post Next Post