MRADI WA KULETA MAENDELEO KWA WATOTO WA KIKE NA VIJANA WASAINIWA


Na Mwandishi Wetu 

Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation, Equity Bank Tanzania pamoja na Equity Group Foundation wameingia makubaliano yanayolenga kuleta maendeleo kwa mtoto wa kike na vijana kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF) ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Wanu Hafidh Ameir wakati wa hafla ya utiaji saini wa Makubaliano hayo iliyofanyika jijini Dar es salaam.


Amesema Mkataba huu utaenda kuiwezesha Taasisi yetu kuleta maendeleo kwa vijana kwa kuongezea ujuzi kupitia VETA, itasaidia katika suala zima la nishati na mazingira kuhakikisha kaya zinapata nishati safi kwa kupikia ili kupunguza uchafuzi wa mazingira” Amesema Mhe. Wanu.


Katika hafla hiyo Mgeni Rasmi Dkt. James Mwangi, CEO wa EQUITY GROUP.MIF ni shirika lisilo la serikali na lisilo la faida lililoanzishwa kwa lengo la kuweka mfumo wa kuunda mazungumzo yanayoweza kutekelezeka, mitandao, habari na kubadilishana ujuzi kuhusu ustawi wa wanawake, vijana na watoto katika afya, elimu na nyanja za kiuchumi za kijamii.


Ubia huo unalenga kuisaidia MIF katika Elimu ya Kifedha na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa makundi yanayolengwa kutoka sekta mbalimbali kama vile Kilimo, Afya, Elimu n.k

Kwenye sekta ya kilimo benki ya Equity imesema itahakikisha wakulima wanakuwa katika mfumo rasmi wa kilimo ili waweze kuhudumiwa mahitaji yao na kuwaongezea mnyororo wa thamani wa bidhaa zao.

Pia Equity benki itasaidia Ujengaji wa uwezo kwa wafanyakazi wa MIF juu ya maswala ya fedha na uandaaji wa ripoti.Itatoa msaada na ushirikiano katika Nyanja za wafanyakazi wenye sifa watakaofanya kazi moja kwa moja


Previous Post Next Post