WAZIRI PINDI CHANA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA UTALII UTAKAO JADILI NAMNA YA KUKUZA SEKTA YA UTALII


Na Lilian Ekonga, Dar es salaam

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana, amefungua mkutano wa Siku mbili ulioandaliwa na Chuo Cha Utalii ambao umeunganisha wadau mbalimbali wa maswala ya utalii kutoka nchi 8 barani Afrika.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kufungua mkutano Huo uliofanyika Jijini Dar es salaam, Waziri amesema Katika mkutano Huo Kuna paper ambazo zitawasilishwa takribani 55 kutoka Kwa wadau wa utalii Katika nchi zisizopungua 8 barani Afrika.

Waziri Pindi amesema kuwa mkutano huo umekutanisha wataalamu wa maswala ya utalii kutoka vyuo ambavyo vinajikita kwenye maswala ya utalii, kutoka taasisi mbalimbali zinazoshughulika na maswala ya utalii na wizara ya utalii wamekutana Kwa pamoja ndani ya Siku mbili kujadiliana namna gani wanapeleka mbele sekta ya Utalii.



"Kuja na mikakati mipya ya kuendeleza Utalii na janga la UVIKO.Mkutano huu ni sehemu ya matunda ya utalii, hivi tumesema Katika mazao mapya ya utalii ni pamoja ya Mikutano ya utalii," Amesema Waziri Pindi.

Aidha Waziri amesema anatoa mualiko Kwa wadau mbalimbali ambao wanataka kuwekeza Katika maeneo Nchini, bado nafasi zipo nyingi hususani Maeneo ya kusini kwajili ya kukuza Utalii Nchini.

"Utalii unachagia Asilimia 17 ya pato la Taifa na Asilimia25 ya fedha za kigeni na Utalii unachagia ajira takribani Milioni 1.5. Utalii ni up Ambayo inaongeza uchumi wa nchi" Amesema Waziri 

Kwa Upande Wake Kaimu Afisa Mtendaji wa Chuo Cha Utalii, Dkt Florian Mtei amesema wameona muda muafaka Kwa Sasa kuitisha wataalamu wa Utalii kuja na matokeo ya tafiti zao ambazo wamefanya mbalimbali Ili waweze kuona Kwa namna gani wanaweza kutokea hapo na kwenda mbele kwenye maswala ya utalii
 
 "Raisi ameonyesha juhudi kubwa baada ya kufufua Utalii kupitia Royal tour baada ya UVIKO na sisi kama Chuo Cha Utalii tuangalia kwa namna gani tunaweza kujikita eneo Moja kwenda lingine kwa kuja na mikakati sahihi ya kiushauri ya namana tunaweza kuendelw kwenye Janga hili la UVIKO19," Amesema Dkt Mtei.

Ameongeza kuwa Wamepata watalaamu wengi sana kutoka Tanzania na nje ya Tanzani na kutakuwa na paper kutoka afrika ya Kusini zaidi 15 na 7 kutoka Kenya na Namibia, Zimbabwe pamoja na Malawi na nchi nyingine.

"Baada ya mkutano huo watakuja na mikakati kabambe ya kuangalia Kwa namna gani wai kama nchi zinzoendelea tunaweza kukabiliana na janga la UVIKO 19 na namna ambavyo tutaweza kuendeleza Utalii wetu na kuwahudumia watalii wetu Kwa viwango vinavyo hitajika,"Amesema Dkt Mtei.
Previous Post Next Post