Na Lilian Ekonga, Dar es salaam
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua matokeo ya Sensa mwishoni mwa mwezi Oktoba 2022 katika tarehe ambayo itatajwa hapo baadae huku maandalizi ya uzinduzi huo yakiwa yanaendelea.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Octoba 12 Kamisaa wa Sensa Anna Makinda amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikamilisha rasmi zoezi la kuhesabu watu,Majengo pamoja na Anwani za Makazi kutokana na hamasa ya wananchi ambayo wameionyesha na kukamilisha zoezi hilo Kwa wepesi.
Alikadhalika Makinda amefafanua zaidi kuwa Sensa ya mwaka huu imetumia teknolojia ya Hali ya juu iliyohusisha matumizi ya vishikwambi katika awamu zote za utekelezaji na kuongeza ubora wa takwimu zilizokusanywa.
"Tangu kukamilika Kwa zoezi la kuhesabu watu,wataalamu wamekuwa wakiendelea na kazi ya Uchakataji wa taarifa zilizokusanywa Ili kupata matokea mbalimbali ya sensa hiyo."
Aidha,Kamisaa ameeleza kuwa Serikali inatoa pongezi na kuwashukuru wananchi wote kwa namna walivyojitoa kuhakikisha Sensa ya watu na Makazi Kwa mwaka huu linafanikiwa.