Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Makumbusho ya Taifa, Dkt. Oswald Masebo akifungua mafunzo ya wajumbe wa Bodi hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga (Katibu wa Bodi) akiwakaribisha Wajumbe wa Bodi hiyo katika mafunzo ya wajumbe hao
Na Mwandishi Wetu
Wajumbe ya Bodi ya Makumbusho ya Taifa wanafanyiwa mafunzo juu ya utendaji wa kazi yao ya kuisimamia menejimenti ya Taasisi hiyo.
Mafunzo hayo yanayoendeshwa na Chuo cha Utumishi wa Umma sehemu ya Global Learning cha jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa, Dkt. Oswald Masebo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassani kwa kumteu kuisimamia Taasisi hiyo.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Dkt Masebo alimshukuru Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi. Dkt Pindi Chana kwa kuwateua wajumbe wa Bodi ya Makumbusho ya Taifa ili kwa pamoja waisimamia menejimenti ya Taasisi hiyo.
Dkt. Masebo ameeleza kuwa Bodi yake iko tayari kushirikiana na menejimenti ya Makumbusho ya Taifa ili kuleta maendeleo ya Taasisi hiyo na kwa Taifa kwa ujumla.
“Sisi kama wajumbe wa Bodi hii tupo tayari kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Makumbusho ya Taifa ili kuleta maendeleo endelevu kwa taasisi hii” amesema Dkt. Masebo.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo ameipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kazi kubwa ambayo wameifanya wakati kukiwa hakuna bodi.
Aimeipongeza Menejimenti ya Makumbusho ya Taifa kwa kuona umuhimu wa kuandaa mafunzo kwa wajumbe wa Bodi hata kabla ya kuanza kazi rasmi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Noel Lwoga amempongeza Mwenyekiti wa Bodi hiyo kwa kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Vile vile amempongeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Balozi. Dkt. Pindi Chana kwa kuwateua wajumbe wa Bodi na kwamba yeye pamoja na menejimenti yake watatoa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha kuwa Bodi inatekeleza majukumu yake.