AUMS yajivunia kutoa ajira kwa watanzania



Na Humphrey Msechu, Geita

MRATIBU wa Maudhui kutoka kampuni ya Afriacan Underground Mining services (AUMS), Tina Kinabo Amesema kuwa kampuni yao inafanya kazi katika mgodi wa GGML na wafanya uchimbaji wa chini ya ardhi na wanatumia mitambo ya kisasa katika ufanyaji kazi na wao ni kampuni ambao wameungana na kampuni nyingine ya kitanzania ambayo inaitwa BG Umoja ambayo inawasaidia katika ufanyaji kazi wao..

Amesema kuwa kampuni yao wafanyakazi wao asilimia 90/ ni wafanyakazi wakitanzania na pia kuna wazungu ambao wanawasaidia kuwapa elimu ya uchimbaji chini ya ardhi vijana wa kitanzania na kazi zao nyingi wanazifanya mgodi wa GGML ambao upo geita na kidogo wanachokipata wanakirudisha kwenye jamii ya mkoa huo.


Tina ameyasema hayo katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari walipotembelea banda hilo lililipo kwenye maonyesho ya tano ya teknolojia na uwezeshaji wa madini yanafanyika mkoani humo ambapo amesema kuwa wanatoa elimu kwa vijana ambao wapo geita na nje ya geita wanawafundisha ,wanawaelimisha,na wanamategemeo makubwa kazi yao wanayoifanya.

"Sisi kama kampuni tunapenda kuishukuru Serikali ya Jamhuru ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kupitia Rais Samia Hassan Suluhu na Rais Mwinyi kwa kazi kubwa wanazofanya.


"Ndugu waandishi wa habari leo tumetembelewa na Mkurugenzi wa Idara ya Nishati na Madini ,Wizara ya Maji , Nishati na Madini Zanzibar Said H Mdungi tunaimani atatufikishia salamu zetu Zanzibar na kupeleka elimu ya jinsi ya kuchimba madini chini ya ardhi.

kwaupande wake Mkurugenzi huyo wa Idara ya Nishati Zanzibar Said Mdungi amesema kuwa kitendo cha kuwapa nafasi wazawa kwenye maeneo mbalimbali katika kampuni hiyo ni moja ya sera ya serikali na malengo ya serikali katika kuwafikia wazawa.

"Nitowe wito kutumia fursa hii ili malengo ya serikali yaweze kufikiwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na nchi yetu."amesema Mdundi
Previous Post Next Post