UZINDUZI WA MRADI WA KIJANA MKAKATI WENYE LENGO LA KUTOA ELIMU KWA VIJANA KUHUSIANA NA MIKOPO


Na Lilian Ekonga, Dar es salaam

Halmshauri ya Manispaaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imewataka vijana walionufaika na mikopo ya halmshauri ya Asilimia 10 mahususi Kwa vijana, wanawake na walemavu kurejesha mikopo hiyo Kwa Muda muafaka kwani hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wasiorejesha mikopo hiyo.


Rai hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Afisa Maendeleo ya jamii Manispaaa ya Kinondoni Furaha libangu, Katika hafla ya Uzinduzi wa mradi wa Kijana Mkakati wenye Lengo la kutoa Elimu Kwa vijana masuala ya uongozi pamoja na usimamizi WA fedha hizo za mikopo zinazotolewa na halmshauri.
  
Ambapo amesema Katika halmshauri hiyo vijana wengi walionufaika na mikopo hiyo hawarejeshi mikopo hiyo kutokana na vijana kuingiwa na Tamaa baada ya kupata fedha hizo.

Pia ametoa rai kwa mashirika mbalimbali kuandaa majukwaa mbalimbali kwa ajili ya kuwajengea uwezo vijana juu ya matumizi sahihi ya mikopo pamoja na kuwaunganisha na fursa zitakazo wakwamua vijana kiuchumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji WA shirika lisilo la kiserikali linalosimamia mradi wa Kijana Mkakati TAYOBECO Shida Kabulunge, amesema mradi Huo utawapa Elimu vijana namna Bora ya usimamizi WA fedha pamoja naa usimamizi WA Miradi ya biashara wanazoanzisha pamoja na Miradi mbalimbali.

"Dhumuni la mradi wa Kijana Mkakati ni kufikia zaidi ya vijana 2000 wa manispaa ya Kinondoni ili kunufaika na fursa za mikopo" amesema shida.

Nae Afisa mradi wa Kijana Mkakati, Innocent Deus Amesema mradi huu unalengo la kuwafikia vijana Katika Maeneo tofauti Ili Kupata Elimu kuhusiana na ujasiriamali pamoja na Elimu ya jinsi ya kuchukua mikopo.
Previous Post Next Post