VETA yaja na suluhisho la kupunguza kemikali katika uzalishaji wa mazao



Na Humphrey Msechu, Mbeya

MTAALAMU wa maabara kutoka chuo cha Veta jijini Dar es Salaam Mwalimu Ally Issa amesema kuwa kupitia maonyesho ya nanenane ambayo kitaifa yanafanyika Jijini Mbeya wao kama wataalamu wa maabara wamekuja na bidhaa ambazo ni suluhisho la kupunguza kemikali katika uzalishaji wa mazao yao mashambani.

Amesema jambo hilo wameona ni muhimu kwa wakulima ili kuweza kupunguza athari ambazo wanazipata wakulima kwa kutimia bidhaa zenye kemikali kama vile dawa za kupuliza mashambani,mbolea na mambo mengine mengi.

Issa ametoa kauli hiyo Agosti 2 Jijini Mbeya kwenye maonyesho ya kitaifa ya nanenane ambayo yanafanyika mkoani humo ambapo amesema wakulima wengi wamekuwa wakilima katika mashamba yao wamekuwa wanaweka majivu ili kurudisha hali fulani ya uoto wa asili nakudai kuwa ukiona mkulima amefikia hatua hiyo basi ujuwe udongo tayari una asidi nyingi.


Amesema kuwa kuharibika kwa udogo kunapeleka mazao kutokukuwa kwa ubora na ili kuondoa hali hiyo ndio maana wamekuaja na mbolea za asili ambazo zimetengenezwa na wao kama wataalamu na ni za maji na matumizi yake ni kama wanavyotumia mbolea walizozizoea.

"Mbolea hizi unaweza kutumia kwa kukuzia na kuoteshea mazao yako pasipo na shaka kabisa  na nimbolea ambazo zinaongeza virutubisho kwenye udongo na kukuongeza uzalishaji mkubwa utakakuwezesha kupata kipato kikubwa"amesema Mwalimu Issa

Ameongeza kuwa wamekuwa na dawa nyingine ambayo inatumika kuondoa magugu mashambani na ni magugu aina yote hivyo wakulima wanakaribishwa na kujongea kwenye banda la veta katika maonyesho ya nane nane yanayoendelea jijini mbeya.



Issa Amesema kuwa licha ya dawa hizo lakini pia wamekuwa na dawa za kuwa wadudu ambao wanashambulia mazao kama vile maharagwe,mahindi ka hiyo waliona kama nishida kwa wakulima na ndio maana wamekuja na dawa hizo ambazo hazina athari zozote kwani dawa hiyo ni asilia.

"Niwakaribishe sana watanzania katika banda la veta ili kupata huduma kupitia chuo chao cha veta ambapo kwa sasa tupo kwenye maonyesho ya nane nane."

Nakuongeza kuwa "wananchi wote hususani mliopo nyanda za juu kusini mfike kwenye maonyesho haya na zaidi kwenye banda la veta ili kujipatia elimu matumizi ya dawa asili kwaajili ya kuboresha kilimo."amesema Issa

Akizungumzia zaidi kuhusu dawa za asili inakwenda kuongeza virutubisho nkwenye udongo na kwenda kuongeza mazao kukua hivyo wananchi wajitokeze wapate suluhu za changamoto wanazokutana nazo kwenye kilimo na waendelee kutumia bidhaa za veta ambazo ni asilia na wapunguze kutumia bidhaa zenye kemikali.
Previous Post Next Post