SERIKALI KUZIDI KUBORESHA MIUNDOMBINU KATIKA SEKTA YA ELIMU NCHINI


Na Mwandishi Wetu 

Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema maboresho ya Miundombinu yanayoendelea katika sekta ya elimu yanalenga kuhakikisha watoto wa kitanzania wanapata elimu inayowapatia ujuzi.


Akizungumza baada ya kuzindua Miundombinu iliyojengwa na kukarabatiwa na Serikali kwa kushirikiana na serikali ya Canda kupitia Mradi wa Kuboresha Vyuo vya Ualimu Nchini, amesema ukarabati huo utakwenda sambamba na uboreshaji wa mitaala pamoja na mapitio ya Sera ya Elimu ya Mwaka 2014.


Akizungumza katika uzinduzi huo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema ukarabati na uboreshaji wa Miundombinu katika Vyuo vya Ualimu ni sehemu ya mikakati ya Wizara ya kuleta mageuzi katika Sekta kwa kuhakikisha elimu inatoa ujuzi il kuandaa wahitimu wanaoendana na soko la ajira la ndani na nje ya nchi.


Prof. Mkenda ameongeza kuwa Wizara inakamilisha Rasimu za Sera na Mitaala ya Elimu Msingi na kwamba Wizara itakuwa na kongamano kubwa litakalofanyika Mwezi wa Kumi la kupokea maoni kutoka kwa wadau juu ya rasimu ya Mitaala na ya Marekebisho ya Sera ya Mwaka 2014.
Previous Post Next Post