ZAID YA WATU 90 KUSHIRIKI KWENYE MBIO ZA PIKIPIKI ZA EAST AFRICA SUN VILLAGE ENDURO RACING.



Zaidi  ya  washiriki  sitini  wanatarajia  kushiriki  mashindano  ya  mbio  za  pikipiki  yaliyopewa  jina  la East  Afrika  Sun Village Enduro Racing 3.

Akizungumza  kuelekea  siku  ya  Mchezo  huo  Mratibu  wa  Mashindano  hayo  ambaye   ni  Mwenyekiti   wa   Dar es Salaam Riders  Motor  Sports Club  ( DRMSC)  Ahmed  Abdallah   amesema  mchezo  huo  unalengo  la  kuwaleta  karibu  wadau  wa   michezo  ya  Mbio  za  Pikipiki  na   kuionyesha  Dunia  kuwa  Tanzania  kuwa  ni  miongoni  mwa  Washindani katika  mchezo  huo.

Aidha  Ahmedi   Abdallah  ameongeza  kuwa  mashindano  hayo  ya  Mbio  za  Pikipiki  ya  Sun Village Enduro  3  yatafanyika  Kibaha  Misugugugu  yakishirikisha  pikipiki  maalum  za  Mashindano  pamoja  na   Bodada  huku  washirki  wakitarajiwa  kupita  na  vyombo  vyao  moto  katika  barabara  za  Mchanga, Tope,  pamoja   na  Matuta  Makubwa .

Sanjari  na  hayo   Mwenyekiti   DRMSC   Ahmed  Abdallah   amesema  mashindano  ya  mchezo  huo  yanatarajiwa  kufanyika  Julai  17,2022  katika  viwanja  vya  Misugusugu  Shule  Kibaha  huku  yakishirikisha  washiriki  kutoka   Mikoa  mbalimbali  ikiwemo   mkoa    wa  Morogoro , Dar es Salaam , Arusha , Pwani  na  Zanzibar .
Previous Post Next Post