TEF yaongeza nguvu kulekea Mabadiliko ya Sheria



JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limeteuwa wahariri sita kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini kusaidia  mchakato wa mabadiliko ya sheria za habari nchini.

Wahariri hao ambao watakuwa na jukumu la kuwasimamia waandishi wa habari waandamizi  kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini ili kujikita katika kuelekea mabadiliko ya sheria ya habari.

Akizungumza wakati wa kikao cha kuteua Kikosi Kazi hicho katika Ofisi za TEF jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Deodatus Balile amesema wanapaswa kuwa na waandishi wabobezi katika harakati hizo, hali iliyopelekea  kuundwa kwa timu ya wanataaluma ambao watawasimamia waandishi ili waweze kupita njia itakayoleta mafanikio.

Amesema uteuzi huo unalenga  kuongeza chachu ya harakati kuelekea mabadiliko ya Sheria za habari nchini.

“Timu hii ya wataalamu wabobezi, itasaidia kwa kiwango kikubwa kunyoosha mwelekeo na hatimaye kupata matokeo chanya,” amesema Balile.


Wahariri hao walioteuliwa na TEF kuwasimamia waandishi (mentors) ni Joseph Kulangwa wa gazeti la Raia Mwema, Stella Aron- Majira, Rashidi Kejo -Mwananchi, Angela Mang’enya wa Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC) pamoja na Wahariri wastaafu Joseph Nakajumo na Midladjy Maez.

TEF imebainisha kuwa Angela Mang’enya amepangwa kuwakufunzi Fatma Hassan Ali (Channel Ten), Kissa Daniel (East Africa TV), Faridy Mohammed (Mlimani TV), Godfrey Monyo (ITV).

Aidha Joseph Nakajumo atawasimamia Christopher James (Radio One), Salma Juma (Classic Fm), Philip Nyiti (Clouds Media) na Brumo Bomola (Radio Tumaini).

Kwa upande wa Rashid Kejo atawaongoza waandishi Regina Mkonde (Mwanahalisi Online), Faraja Masinde (Mtanzania Digital), Brighter David (Daily News Digital) na Iddy Lugendo wa Majira.

Joseph Kulangwa amepangiwa Alex Kazenga (Jamhuri Media), Peter Elias (Mwananchi), Mery Geofrey (Nipashe) na Goodluck Hongo wa Tanzania Daima.

Waandishi wengine ni Anneth Nyoni (Tumaini TV), Humphrey Msechu (Sparklight TV), Jackline Martin (Times Majira) na Yusuph Digossi (IBN TV) watakuwa chini ya Stella Aron

Kwa upande wa Maez atakuwa na kazi ya kupitia kazi na kuandika ripoti.

Previous Post Next Post