RITA YAANDA MKUTANO NA WADAU MBALI MBALI"WAZIRI NDUMBARO MGENI RASMI".



Wakala wa Usajili, ufilisi na Udhamini RITA  wameandaa Mkutano na wadau mbalimbali ambao umelenga kujadili  na kuchakata kwa pamoja namna bora ya kutoa huduma kwa wananchi kwa Lengo la kutadhimi walipotoka, walipo na wanapoelekea.

 Akizungumza na waandishi wa  habari,Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu RITA, Angela Anatory amesema Mgeni Rasmi  wa Mkutano Huo atakuwa waziri Katiba na Sheria Mhe, Dkt Damas Ndumbaro, na  mkutano huo  utafanyika July 18 katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam. 

Amesema kuwa, Katika Mkutano huo utahudhuriwa na viongozi wa Dini, Wizara mbalimbali, Taasisi za Serikali mabalozi mbalimbali pamoja na wadau wengine ambapo miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa ni pamoja na mafanikio walioyapata, Changamoto pamoja na kujiwekea mikakati ambayo itasaidia kuzitatua na kusonga mbele.



Hata hivyo, ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutumia huduma mbalimbali zinazotolewa na Rita ikiwemo kufilisi na kudhamini, kusajili Talaka,  ndoa, vyeti vya vizazi na vifo, kusimamia mali ambazo hazina mwenyewe, na za watoto ambao hawajafikisha miaka 18, kusajili mirathi, kuwasili watoto pamoja na kuandika wosia.

"Kumekua na changamoto nyingi za watu kutopata mali zao baada ya watu wanapoachana ama kufariki, ndio maana tunataka tukae pamoja tujadili namna bora ya kuweza kutatua changamoto hizi, tunafanyakazi kwa kushirikiana na watu wa Ustawi wa Jamii tupo nao karibu kuhakikisha mambo yote yanakwenda vizuri"amesema Angela.

Aidha Amesema Moja ya mafanikio walioyopata RITA ni kubuni Programu ya usajili wa watoto chini ya miaka 5 ambapo mpaka Sasa wamefanikiwa kuongea kiwango Cha usajili kutoka asilimia 13 mpaka asilimia 65 na kufikia watoto Milioni 7 waliosajiliwa katika mikoa 23 ya Tanzania Bara.




Previous Post Next Post