MARENGA: SHERIA YA UHALIFU WA MITANDAO IMEVURUGA UHURU WA FARAGHA



Na Humphrey Msechu 

Imeelezwa kuwa Sheria ya Uhalifu  wa mitandao kupitia Kifungu cha  7 iliyotungwa mwaka 2015 imevuruga uhuru wa faragha ambapo taarifa binafsi za mtu zinaweza kuchukuliwa na polisi kinyume na Ibara ya 16(i) ya Katiba ya Tanzania.

Hayo yamebainishwa  leo  Julai 20 na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA – TAN) James Marenga alipokua akizungumza katika Semina ya waandishi wa habari za mtandaoni iliyofanyika Jijini Dar es salaam.

Marenga amesema kuwa  Sheria hii katika Kifungu cha 50(2)(b) kinaondoa haki ya mtu kukata rufaa kinyume na Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba, lakini pia Kifungu cha 38(2)(b) cha sheria hii kinaruhusu usikilizwaji wa shauri mahakamani hata bila muhusika kuwepo.


“Hukumu ikitolewa, ndio unatafutwa na kufungwa bila kujua kesi yako ilipelekwa mahakani lini, na kwa kosa gani” Amesema Marenga 
Katika hatua nyingine Marenga amebainisha kuwa sheria Uhalifu wa Mtandaoni iliyotungwa Mwaka 2015, imebeba maneno yenye ukakasi na hatari zaidi kwa wanahabari kwasababu kwenye sheria hiyo kuna adhabu zilizowekwa kwa makosa ambayo hayapo wazi kinyume na Ibara ya 13 (6)(C) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“kupitia Kifungu 7 (i)(g) iliyotungwa mwaka 2015, imevuruga uhuru wa faragha ambapo taarifa binafsi za mtu zinaweza kuchukuliwa na polisi kinyume na Ibara ya 16(i) ya Katiba ya Tanzania”
Kwa upande wake Mwenyekiti wa jukwaa la Wahariri Tanzania Deodatus Balile amesema wadau wa habari wanapopigania  sheria hii  iondolewe ama ipitiwe upya, ni kwamba watu wajue wanapigania maslahi ya wengi .


Amesema , baadhi ya vipengele vya sheria hiyo  vinapaswa kuondolewa kabisa kutokana na kuwa na matatizo ikiwemo kuruhusu kesi ya mwanahabari kuendeshwa bila ya yeye kujua. 
‘’Sheria inaruhusu kesi yako kuendeshwa bila wewe mwenywe kujua. Kesi unaweza kufunguliwa Mwanza, siku unashuka mtaani unakutwa unapigwa tanganyikajeki” amesema Balile.
Previous Post Next Post