BARAZA la Tiba Asili na Tiba Mbadala Tanzania, limepiga marufuku matumizi kwa binadamu dawa aina ya Hensha maarufu Mkongo, inayomilikiwa na kituo cha Nyasosi Traditional Clinic cha jijini Dar es Salaam na kuifutia usajili dawa hiyo.
-
Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Prof. Hamisi Masanja Malebo, ametoa kauli hiyo leo Julai 27, 2022 mjini Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari.
-
Profesa Malebo alisema baraza katika uchunguzi wake, lilibaini dawa iitwayo Hensha maarufu Mkongo, yenye usajili namba TZ17TM0027, ilikutwa imechanganywa na dawa ya kisasa ya nguvu za kiume iitwayo sildenafil, kwa jina maarufu la biashara Viagra ama Erecto.
-
Alisema kitendo hicho ni kinyume cha sheria na miongozo ya usajili wa dawa za tiba asili na mbadala.
-
Alisema kituo hicho kimetakiwa kuhakikisha kinaiondoa sokoni mara moja dawa hiyo, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mmiliki.
-
Una maoni Usisite kutuandikia