Tanzania imeshiriki katika Mkutano wa 26 wa Wakuu wa Nchi na serikali ya Jumuiya ya Madola(CHOGM) uliofanyika Kigali, Rwanda kuanzia trarehe 19hadi 25 Juni 20 ambao uliongozwa na Makamu w Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ambaye alimwakilisha Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuhairishwa Mara Mbili mwaka (2020, 2021).
Hayo ya mesemwa Leo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula wakati akitoa taarifa kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mkutano huo, amesema kutokana na Janga la UVIKO 19 linaendelea kuitesa dunia hadi sasa moja wapo ya mijadala ya mkutano huu ilikuwa ni namna gani dunia itakavyoweza kujikwamua kiuchumi na kijamii kutokana na janga hili.
Waziri Amesema mkutano huu wa 26 ulihudhuriwa na Wakuu wa Serikali 27 kati ya nchi 54, ambapo wakuu wengine wa Serikali wapatao 27 na mkutano ulijikita kwenye maeneo makuu ya kipaumbele cha utawala bora, utawala wa sheria na haki za binadamu; vijana, afya,teknolojia na uvumbuzi; na uendelevu kwenye masuala ya uchumi, biashara, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na utunzaji wa mazingira.
Pia Amesema Mkutano CHOGM ulijumuisha matukio mengi yakiwemao jukwaaa la biashara katika kujadili fursa za biashara na uwekezaji kwenye jumuiya ya madola na Bara la Afrika na Changamoto mbali mabali zinazokabili sekta hizo, jukwaaa la wanawake na jukwaaa la vijana.
Hata hivyo Waziri Amesema katika Mikutano huo, Mawaziri wa Mambo ya Nje, walikutana kwenye mikutano miwili, mmoja ulijadili Mkutano wa Wakuu wa Serikali na mwingine ulizungumzia masuala mbalimbali yanayohusu nchi ndogo na Kwa upande wa Mkutano wa Mawaziri kuhusu nchi ndogo uliofanyika chini ya Uenyekiti wenza wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda na St. Vincent and Grenadines.
"Ulijadili changamoto za nchi ndogo hususani kufuatia janga la UVIKO-19, athari zinazotokana na mabadiliko ya tabianchi na mgogoro unaoendelea kati ya Urusi na Ukraine pamoja na upatikanaji mdogo wa fedha za maendeleo"
Waziri amesema Kwa upande wa Mhe. Makamu wa Rais alifanya mazungumzo na Bi. Melinda Gates, mwanzilishi mwenza wa taasisi ya Melinda and Bill Gates na kuishukuru taasisi hiyo kwa kuendelea kusaidia Tanzania katika kuboresha sekta ya afya ikiwemo kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza kupitia tafiti.
"Vilevile, Mhe. Makamu wa Rais alieleza ukubwa wa changamoto ya malaria nchini Tanzania ambapo alifafanua kuwa zaidi ya asilimia 94 ya wananchi wapo kwenye hatari ya maambukizi ya ugonjwa huo".
Aidha Amesema Mhe. Makamu wa Rais alifafanua jitihada za kukabiliana na malaria ikiwemo Mkakati wa Taifa wa Mwaka 2021-2025 unaolenga kupunguza maambukizi ya malaria hadi kufikia chini ya asilimia 3.5 ifikapo mwaka 2025 na kutokomeza kabisa ugonjwa huu ifikapo mwaka 2030.