KAMPUNI YA NGASMAKE YAJA NA SULUHISHO LA CHANGAMOTO ZA KIUSALAMA KUPITIA BISHARA YA MTANDAO" LIPA KWA UHAKIKA"


Kufuatia changamoto za kiusalama katika biashara za kimtandao ( Online Business) kwa mnunuzi na muuzaji ikiwemo udanganyifu na utapeli katika biashara pamoja na mnunuzi kupata huduma au bidhaa isiyo na kiwango kampuni ya NGASMAKE Co. Ltd imekuja na suluhisho la kutatua changamoto hii baada ya kuzindua mfumo salama wa LIPA KWA UHAKIKA .

Mfumo huu umeripotiwa kuwa utamsaidia mnunuzi na muuzaji kuwa salama katika biashara za mtandao ( online Business) na kuondoa changamoto ya udanganyifu,  utapeli na bidhaa zisizokuwa na kiwango.



Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo uliofanyika katika Ofisi za Shirika la Mawasiliano  Tanzania (TTCL) Jijini Dar es salaam  Mkurugenzi Mtendaji wa NGASMAKE CO LTD , Emmanuel Ngalya amesema kuwa huduma hiyo ni ya kipekee hapa nchini ambayo inatoa usalama kwa wauzaji na wanunuzi wa bidhaa na huduma kimtandao. 

" Kuwepo kwa changamoto za kiusalama katika biashara za kimtandao haswa utapeli na mnunuzi au kupata bidhaa isiyo na kiwango ndio sababu ya kampuni yetu kuja na suluhisho la mfumo huu rafiki ambao utamsaidia mnunuzi na muuzaji kuwa salama katika Biashara " Amesema Bw. Ngalya

Kwa upande wake Mkurugenzi wa T-PESA kutoka TCCL, Bi  Lulu mkudde  amesema huduma hiyo itaondoa kilio cha muda mrefu cha wanunuzi wa bidhaa kutopata bidhaa zoa ikiwa tayari wamekwishafanya malipo.



Ameongeza kuwa kampuni ya NGASMAKE imekuja na suluhisho ya kuja na mfumo Rafiki ba salama wa LIPA KWA UHAKIKA utakaomsaidia Mnunuzi na Muuzaji kuwa Salama katika biashara za mtandaoni na kuondoa udanganyifu na utapeli.







Previous Post Next Post