Utambuzi wa watu wenye ulemavu ulianzia katika azimio la Arusha la mwaka 1967, kuwa miongoni mwa makundi machache yanastahili usaidizi toka kwa jamii. Mwaka 1982 zilitungwa sheria mbili za watu wenye ulemavu
1. Sheria No.2 ya ajira kwa watu wenye ulemavu na
2. Sheria No.3 ya matunzo na huduma kwa watu wenye ulemavu.
Sheria ya ajira ilimtaka kila mwajiri kuhakikisha anaajiri watuwenyeulemau 2%katiyawaajiriwaaliokuwanao. Na sheria ya matunzo iliitaka serikali na jamii kutoa matunzo kwa watu wenye ulemavu ikiwemo matibabu. Japo Sheria ya 1982 ilifutwa na sheria mpya ya watu wenye ulemavu ya 2010; kifungu cha 14 kilianzisha Register ya waajiri ili kuwezesha hatua ya ufuatilia utekelezaji wa Ajira- Wengi waliajiriwa. Kamishna wa ajira alikuwa na mamlaka wakati wowote kuingia sehemu yoyote ya kazi na kuhoji utekelezaji wa ajira kwa watu wenye ulemavu.
Haki ya Ajira kwa watu wenye ulemavu kama vifungu vya sheria vinavosema ( Kfg 31-34:
- Watu wenye Ulemavu wenye vigezo (minimum qualifications) wana haki ya kuajiliwa
- Kila taasisi yenye waajiliwa kuanzia 20 asilimia 3 wanapaswa kuwa na watu wenye ulemavu
- Utaratibu wa ajira unapaswa kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu
- Mwajiri anapaswa kuweka mazingira rafiki kwa mtu mwenye ulemavu
- Waajiri wote nchini wanapaswa kila mwaka kutoa taarifa kwa kamishna wa kazi juu ya hali ya ajira kwa watu wenye ulemavu katika taasisi yake 31(4)
- Kuhakikisha waliopata ulemavu kazini ajira inalindwa, wanawekewa ,mazingira ya kuendelea na kazi