CHUO CHA MAJI KUFANYA ZOEZI LA UPIMAJI WA SAMPULI ZA MAJI YA VISIMA BURE KWA WAKAZI WA DAR.


Kutokana na Umuhimu wa Kila mwananchi kuwa na haki ya kutumia maji safi na Salama Chuo maji kimetangaza kutoa Huduma ya Upimaji wa sampuli za maji ya visima   vinavyotumika kwa matumizi ya nyumbani  bure kwa wakazi mia moja (100) wa Mkoa  Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi Habari Mkuu wa Chuo Cha Maji Adam Karia, amesema  kufuatia Maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma yaliyoanza  Tarehe 16 hadi 23 ya mwezi wa sita wameamua  kurudisha Huduma  kwa jamii kwa kufanya zoezi la Upimaji wa sampuli za Maji ya visima bure ambapo Kila sampuli moja inagharimu kiasi Cha shilingi laki moja na tisini(190,000) ikujumuisha Upimaji wa vigezo vyote ambavyo vimeelekezwa na shirika la viwango Tanzania TBS.




Amesema Watapokea taarifa  kwa wale watakopenda kushiriki katika Huduma  hii inayoanza  Tarehe 16 ya mwezi wa sita mpaka pale idadi ya sampuli 100 zitakapo kamilika, ambapo mshiriki anatakiwa kupiga simu kwenye namba 0718 968582 au 0621 879079 na kutoa taarifa sahihi ikiwemo  jinsi ya wataalumu wao kukufikia na kuchukua sampuli ya maji kwaajili ya Upimaji

Aidha Amesema wanamshukuru Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani Kupitia Waziri wa Maji Juma Aweso wameweza Kupata Fedha shilingi Bilioni Moja na Nusu waliyoiomba kwa ajili ya ukarabati wa Majengo ya Hostel za wanafunzi wa Chuo Cha Maji zilizipo chuoni Hapo.

Previous Post Next Post