WATOTO zaidi ya Laki 7 wa Mkoa wa Dar es Salaam, walio chini ya umri wa miaka 5, wanatarajiwa kufikiwa kwenye kampeni ya Polio ya matone awamu ya Pili zoezi litakaloanza kuanzia tarehe 18-21Mei, mwaka huu ndani ya Wilaya zote 5.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam wakati wa semina ya kuwajengea uwezo juu ya Polio ya matone kwa Waandishi na Wahariri wa vyombo vya Habari, Mratibu wa Chanjo Dar es Salaam, Bw. Juma Haule,
Alisema zoezi linatarajiwa kuanza rasmi 18 hadi 21 Mei ambapo watoto zaidi ya Laki Saba wanatarajiwa kufikiwa nyumba kwa nyumba.
"Tunaelekea kwenye kampeni ya chanjo ya Polio ya matone awamu ya pili, ambapo awali waliendesha mikoa ya pembezoni ikiwemo Njombe, Ruvuma, Mbeya lakini zoezi hilo kwa sasa linaenda Kitaifa zaidi kwa kuwafikia watoto wa mikoa yote.
"Kwa Dar es Salaam tunatarajia kuwafikia watoto zaidi ya Laki Saba kwa kuwapatia chanjo hii ya kuzuia magonjwa ya kupooza." AmesemaJuma Haule.
Na Kuongeza kuwa wanaenda kuwafikia watoto maeneo yote, nyumba kwa nyumba, lakini pia mashuleni, lakini pia maeneo ya michezo, sehemu za fukwe na maeneo yote ambapo walipo watoto." Alieleza Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Haule.
Kwa upande wake, Afisa Mradi wa Mpango wa Taifa wa Chanjo, Bi. Lotalis Gaudau alibainisha kuwa, hadi sasa jumla ya Magonjwa 12 yanazuiliwa kwa chanjo yapo katika Mpango huo wa Taifa wa Chanjo.
Pia ugonjwa huu uathiri watu wa rika zote lakini watoto wadogo uathirika zaidi..ugonjwa huu hauna tiba, lakini unaweza tu kuzuiliwa tu kwa kupata chanjo ya matone ya Polio au ya sindano." alisema Gadau.
Na kuongeza kuwa, tayari chanjo zaidi ya Milioni 13 za Polio zimeshafika nchini na wanatarajia kutoa kwa watoto wa umri wa chini ya miaka 5 kwa nchi nzima.
"Tunatarajia kuwafikia watoto zaidi ya Milioni 10 kwa nchi nzima, tutazindua zoezi letu Kitaifa ambapo tumejipanga kutoa chanjo hiyo nyumba kwa nyumba na maandalizi yamekamilika huku wadau mbalimbali wakiwa wameshirikishwa"amesema Gadau.
Ugonjwa huo wa Polio umekuwa na viashiria mbalimbali ikiwemo ulemavu wa ghafla, tepetepe kwa viungo kama mikono ama miguu, kulegea kwa kiungo kukosa nguvu, kushindwa kunyanyua miguu ama mikono, mtoto kushindwa kukaa, kushindwa kutembea/kuchechemea, kuvuta mguu na mengine mengi.
Aidha, kampeni hizo zinakuja kufuatia kuibuka kwa mgonjwa wa polio, Lilongwe, Nchini Malawi mnamo Februari 17, mwaka huu hivyo, Wizara ya Afya ikaonelea kuchukua juhudi za haraka ilikulinda wananchi wake zaidi dhidi ya ugonjwa huo wa Polio.
Kaimu Mkuu wa kitengo Cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya afya Catherine Sungura akizungumza leo Mei 11 jijini Dar es Salaam wakati wa semina maalum iliyoandaliwa na Wizara ya Afya kwa Wahariri, waandaji wa vipindi pamoja na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu utoaji chanjo ya Polio kwa njia ya Matone Watoto wenye umri chini ya miaka mitano nchi nzima kuanzia Mei 18 hadi 21 mwaka huu.




