Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Saba ya wiki ya Utafiti na Ubunifu katika Chuo kikuu Cha Dar es salaam yatakayoanza jumanne tarehe 24 Mei Hadi Alhamisi tarehe 26 Mei 2022 kuanzia saa 2 Asubuhi mpaka 10 jioni katika Maktaba Mpya. Kampasi ya Mwalimu Julius Nyerere
Akizungumza na waandishi wa Habari Makamu Mkuu wa Chuo, Prof William Anangisye amsema katika Siku ya ufunguzi kutakuwa na wazungumzaji wakuu wawili ambao ni mfanya biashara Ndugu Seif Ali Seif, Mkurugenzi Mkuu wa superdoll Ltd amabe atatoa mada kuhusu Ushirikiano wa sekta ya uzalishaji na vyuo vya Elimu ya juu nchini Tanzania.
Amesema Chuo kikuu Cha Dar es salaam kitatumia fursa hii kujipambanua katika Utafiti ambao ni mojawapo ya majukumu yake makuu kwa kuonesha shughuli zake za Utafiti, Ubunifu, Huduma kwa jamii na ubadilishaji maarifa Kama njia ya kutatua changamoto mbalimbali zinazo kabili jamii nchini hasa katika malengo ya serikali.
Aidha Amesema Kati ya Utafiti na Ubunifu zaidi ya ya 300 , mwaka huu chuo kitaonyesha mirad 103, iliyofanya vyema zaidi Kama vile mradi wa maabara ya kidijitali.
" Maadhimisho haya pia hutoa Fursa ya kuimarisha Ushirikiano baina ya chui kikuu Cha Dar es salaam na wadau mbalimbali kitaifa na kimataifa na kwa kuzingatia Hilo, Siku ya pili ya Maadhimisho, jumatano tarehe 25 Mei 2022, kuanzia saa 2 Asubuhi kutakuwa na Majadala Maalumu wa Ushirikiano ya Kimkakati utakaoshirikisha wadau kutoka katika sekta binafsi na za Umma"Amesema Prof William.
Pia amesema wiki ya Maadhimisho ya Utafiti na Ubunifu itatumika pia kutambua michango iliyotukuka ya wataaluma na wanafunzi wa Chuo kikuu Cha Dar es salaam katika Utafiti, Ubunifu na ubadilushaji wa maarifa.
Amesema Maadhimisho haya yatafugwa tarehe 26 Mei 2022 na Waziri wa Elimu, sayansi na Teknolojia Mhe, Profesa Adolf Faustine Mkenda atawatunuku tuzo watafiti na wabunifu Bora katika makundi tofauti tofauti.