Na John Mapepele
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo.Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema kesho ni siku maalum kwa watanzania kushuhudia na kupiga picha na kombe la dunia na kutazama Filamu ya Royal Tour uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mchengerwa ametoa kauli hiyo leo Mei 31, 2022 kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari akiwa na ujumbe wa FIFA ulioleta kombe hilo nchini.
Amesema Tanzania imebahatika kuwa miongoni mwa nchi tisa za Afrika ambazo kombe hilo linapita na kutoa wito kwa watanzania kutokeza kwa wingi kuja kupiga nalo picha.
Amesema milango shughuli ya kupiga picha na kombe itaanza saa tatu asubuhi hadi majira ya saa 11 jioni na baada ya hapo filamu ya Royal Tour ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Samia Suluhu Hassan ameshiriki itawekwa.
Aidha amesema kwa taratibu za FIFA atakayeruhusiwa kulishika pekee ni Mhe. Rais.
Ameongeza kuwa ujio wa kombe hilo ni fursa ya kuitangaza Tanzania kwa kuwa macho na masikio ya mamilioni ya watu wanafuatilia ziara ya kombe hilo.
Hii ni mara ya nne kwa Tanzania kulipoke kombe la dunia ambapo katika ziara ya sasa Kampuni ya Coca Cola ndiye Mdhamini Mkuu.