Jeshi la Polisi limewakamata wanawake na mabinti 17 wanaotuhumiwa kujihusisha na mtandao unaofanya matendo maovu ikiwemo wanaocheza Vibao kata na Vigoma hasa katika nyakati za usiku katika maeneo Mwanyamala, kinondoni,Mkwajuni, Tandale, Sinza, Buza na Magomeni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe, Jumanne Sagini Amesema Watu hao Wamekuwa wakikeuka Sheria, Mila, Desturi na Maadili mema ya watanzania huku wa kiwa wanatangaza matendo hayo kwa kuyaweka katika mitandao ya kijamii wakihamasisha wengine wafanye matendo hayo.
"Uchuzunguzi uliofanywa na vyombo vya Dola umebaini kuibuka kwa baadhi ya wanawake wanaofundishana matendo ya ngono kwa kutumia vifaa hatarishi Kama chupa za bia soda, mahindi ya kuchoma , ndizi na matango na Baadhi wameunda makundi ya whatsap Ili kuweka picha zao za utupu na wengine kuziweka katika mitandao tofauti ya kijamii"Amesema Naibu Waziri
Aidha Amesema serikali itafuatilia kw karibu mtandao unaowafirishwa watu kwenda ughaibuni ambapo hawapati kazi wanazoahidiwa badala yake hutumikishwa kufanya kazi hatarishi kwa Afya za uhai wao zikiwemo ukahaba na ubebaji madawa ya kulevya na kazi zingine za Ndani.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa maendeleo ya jamii , jinsia , wanawake na Makundi Maalumu, Mwanaidi Ali Khamisi ametoa onyo kwa wale ambao wanatekeleza vitendo vya udhalilishaji dhidi ya wanawake na watoto na kuwataka waache Mara moja endapo wakikamatwa watachukuliwa hatua Kali za kisheria.
Nae kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Jumanne Muliro amesema watuhumiwa 17 waliokamatwa watafikishwa mahakamani na watasimamia kwa karibu kesi hii mpka watakapo kuchukuliwa hatua za kisheria Ili iwe fundisho kwa wengine.