WAZIRI PROF. ADOLF MKENDA AKABIDHI KOMPYUTA 3000 KWA SHULE NA VYUO VYA UALIMU NCHINI



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Pro. Adolf Mkenda ametoa wito kwa wadau wa elimu nchini kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhamasisha matumizi ya TEHAMA kwenye sekta ya Elimu ili kuendana na kasi ya maendeleo ya Sayansi na Teknolojia

Waziri Mkenda ametoa wito huo wakati wa tukio la ugawaji wa kompyuta kwa ajili ya wadhibiti ubora wa shule, vyuo vya elimu na shule za Sekondari nchini, zoezi lililofanyika Jijini Dar es Salaam.


Amesema kuwa hatua hiyo ni dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhamasisha matumizi ya TEHAMA katika shule za msingi na sekondari pamoja na vyuo vya ualimu ili kuendana na kasi ya maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.


Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Caroline Nombo amesema kuwa Tanzania haiwezi kubaki nyuma katika maendeleo ya Sayansi na Teknolojia Duniani hususan katika matumizi ya TEHAMA hivyo zoeli hilo ni moja ya mkakati wa Serikali kupitia Wizara ya Elimu kuendana na kasi ya maendeleo.

Takribani kompyuta 3000 zikijumuisha kompyuta mpakato (Laptop), Desktop zaidi ya 1,000, printer 12 na swichi za Intaneti 12, vimenunuliwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau kwa lengo la kusapoti sekta ya elimu nchini.




Previous Post Next Post