Na. John Mapepele
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe, Kassim Majaliwa Majaliwa kesho Aprili 5, 2022 anatarajia kuwa Mgeni Rasmi kwenye kikao kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo Tanzania Bara jijini Dodoma.
Haya yamesemwa leo Aprili 4, 2022 na Katibu Mkuu wa Wizara. Dkt, Hassan Abbasi wakati akiwa Mwenyekiti wa kikao kazi hicho.
Dkt Abbasi amesema kada za maafisa Utamaduni na Michezo ni kada za kimkakati kwa maendeleo ya nchi yetu.
Aidha, amesema kikao kazi hiki kimetuja katika wakati mwafaka ambapo lugha adhimu ya kiswahili imepata msukumo mkubwa duniani na sanaa imekuwa kazi ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kwenye ajira kwa vijana.
Kwa upande wa Michezo amesema ni wakati ambapo Michezo imepiga hatua kubwa.
Ameyataja baadhi ya mambo kuwa ni pamoja na kushiriki kwenye mashindano makubwa ya jumuiya ya madola na mashindano ya dunia ya mpira wa miguu kwa wenye ulemavu.
Ametumia muda huo kuipongeza timu ya simba kwa kufuzu kuingia robo fainali ya mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Afrika.
Kikao hicho kinahudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka TAMISEMI, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kesho wakati wa ufunguzi raamj kitarushwa mbashara na TBC na vyombo mbalimbali na mitandao ya kijamii


