Mhe. Mchengerwa aahidi makubwa kwenye mechi ya Simba na Orlando Pirates leo



Waziri wa Utamaduni,p Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa  ametoa wito kwa wananchi kujitokeza  kwa wingi kuja kuishangilia timu ya Simba kwenye mchezo dhidi ya timu ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza wa hatua ya Robo Fainali ya mashindano ya Shirikisho la Africa (CAF) unaofanyika leo  Aprili 17, 2022 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa ili kupata matokeo mazuri.

Mhe. Mchengerwa ameyasema haya leo aliposhiriki kwenye mashindano makubwa zaidi ya Quran barani Afrika yanayofanyika kwenye  uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

Amesema mshangiliaji ni mchezaji wa 12 wa timu yoyote hivyo ni muhimu kwa watanzania kujitokeza  kuisaidia Simba ishinde kwa kishindo nyumbani ili kuniweka katika nafasi nzuri.



Mhe. Mchengerwa amewataka watanzania kuiombea timu ya simba ili iweze kuchukua kombe na kulibakiza nchini.

Aidha, ametumia  nafasi hiyo kuwatakia waumini wa kiislamu mfungo mwema katika kipindi hiki cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani pia amewatakia waumini wa kikristu heri ya Sikukuu ya Pasaka leo wakati wanapoadhimisha siku ya kufufuka kwa Yesu Kristo.



Ameongeza kuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa leo, unatumika kwa shughuli kuu mbili ambazo ni mashindano makubwa zaidi ya Quran Barani Afrika yanayomalizika mchana na mchezo wa Simba ambao utaanza saa moja usiku.


Tunawatakia kila la heri na mafanikio katika safari ya kuliwakilisha taifa kimataifa



Previous Post Next Post