Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikiria mtu mmoja kwa kosa la mauaji. Kwamba Mnamo tarehe 20/04/2022 majira ya saa 07:45 mchana huko maeneo ya Mkoani "B" Wilaya ya Kibaha na Mkoa wa Pwani.
Dawiya Iddy Mshihiri, miaka 30, mfanyakazi wa kazi za ndani aliuawa kwa kushambuliwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kitu chenye ncha kali na me (jina limehifadhiwa), miaka 27, msukuma, mfanya kazi wa kulisha mifugo katika nyumba ya Bw Samwel Joseph Kundai.
Mtuhumiwa baada ya kutenda tukio hilo alijaribu kujiuwa kwa kunywa sumu lakini hakufanikiwa kutimiza lengo lake, kwakuuwa alikuwa ameathirika na sumu hiyo alikamatwa kupelekwa Hospital ya Rufaa ya Tumbi kwa matibabu akiwa chini ya ulinzi wa Polisi, mtuhumiwa na marehemu wote walikuwa wanafanya kazi katika nyumba ya Bw.Samwel Joseph Kundai.
Jeshi la Polisi Pwani linaendelea na uchunguzi wa tukio hili, mara baada ya uchunguzi kukamilika mtuhumiwaatafikishwa mahakamni kwa hatua za kisheria.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linatoa rai kwa wananchi wote kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, endapo kutakuwa na tatizo lolote watoe taarifa sehemu husika kwa msaada zaidi.
