WAZIRI DKT. ASHATU KIJAJI : SERIKALI YATENGENEZA JUMLA YA AJIRA 62,401 NA KUSAJIRI MIRADI MIPYA 294 KWA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA WA UONGOZI WA RAIS SAMIA



Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji leo March 10, 2022 amezungumza na waandishi wa Habari kuelezea mafanikio ya Wizara kwa kipindi cha Mwaka mmoja chini ya Uongozi wa Rais samia. Na hivi ni baadhi ya mafanikio ya Wizara hiyo ndani ya mwaka Mmoja

-Katika kipindi cha mwaka mmoja wa serikali ya awamu ya Sita, imewezesha usajili wa miradi 294, ambayo itatengeneza jumla ya ajira 62,401 kwa Watanzania. 

-Hekta milioni 1.6 imetengwa kutoka kwenye ardhi inayomilikiwa na serikali ili kuweka miundombinu wezeshi kwa ajili ya uwekezaji. 

-Katika kipindi cha mwaka mmoja wa serikali ya awamu ya Sita, wizara imefanikiwa kuanzishwa kwa dirisha moja la uwekezaji, ili kukwepa tatizo la urasimu, ambapo muwekezaji atapata kibali ndani ya muda mfupi. 

-Rais Samia Suluhu Hassan kupitia diplomasia ya uchumi amefanikisha kuanza kwa ujenzi wa kongani za viwanda Kigamboni, wenye ukubwa wa wa mita za mraba mil 2.2 utakaogharimu dola za kimarekani milioni 400, ambapo eneo hilo litakuwa na viwanda 100 na kuzalisha zaidi ya ajira 50,000. 

-Serikali ya awamu ya Sita, imefanikiwa kupatiwa ufumbuzi kwa vikwazo 42 vya kibiashara kati ya vikwazo 64 vilivyokuwepo. 

-Serikali ya awamu ya Sita imerahisisha upatikanaji wa vibali vya ajira za wageni, pia imeruhusu wawekezaji kuleta wataalam 10 kutoka nje ya Tanzania, ili wanapokuja kufanya kazi Tanzania wawape ujuzi walionao Watanzania kwa ajili ya manufaa ya Taifa letu. 

-Katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan, jumla ya viwanda 327 vimeanzishwa,  ambavyo ni viwanda vidogo, vya kati na vikubwa. 

-Serikali imewezesha upatikanaji wa majengo mapya Matano kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vidogo vidogo vya wajasiriamali wadogo. Majengo hayo yamejengwa, mkoa wa Katavi (majengo 2), Mwanza (jengo 1) na Morogoro ( majengo 2). 

-Jumla ya Wajasiriamali  4156 (Wanaume 1662 na Wanawake 2494) wamefikiwa na kupewa elimu ya biashara ya namna ya kutumia mikopo halali.
Previous Post Next Post